Thursday 23 May 2013

TABIA


TABIA MBAYA NA TABIA NZURI
Tabia ya mwanadamu ina sura nyingi , kila mtu anajinsi alivyo zaliwa au kujifunza . katika somo hili tutakua tukiangalia mambo yanayo fanana kati ya tabia mbaya na tabia nzuri, na mwisho wa somo hili utagundua kwamba tabia yako iko katika hali gani n ahapo utaweza kufanya maamuzi ya kufikiria tofauti

Tabia huwa inajitokeza mara kwa mara unaweza ukasema mimi tabia yangu haiwezi kufahamika, lakini tabia yako iwe mbaya au nzuri mtu mwingine ataifahamu kwa sababu itajitokeza mara kwa mara, waweza kuwa mvutaji wa sigara, au mnywaji wa pombe, au madawa ya kulevya au mwizi au mtu mkarimu, mcheshi,nk hivi vyote vinajidhihirisha mara kwa mara.

Tabia yako iwe mbaya au nzuri , mtu mwingine aweza kuifahamu kwa sababu haihitaji nguvu nyingi kugundua jinsi ulivyo katika jamii, hivyo itategemea jinsi unavyo penda ufahamike. Mtu aweza kusema kuna haja gani kufahamika? ulimwengu huu unahitaji watu wa pekee ambao watakuwa msaada kwa familia , makanisani, Maofisi ya serikali, nk. watu watapenda kupata wasifu wako, usishangae unaomba kazi mahali unakataliwa , hii ni jinsi ulivo amua kuyaweka maisha yako kwa hiyo ni vyema ukaanza kutengeneza tabia yako iliisomeke kwa faida yako na ya jamii.

Tabia yako inatambulisha nini kipo ndani yako. Ni rahisi mtu kujua tabia iliyomo ndani yako kabla haijajitokeza, kumekuwepo wakati fulani mtu hataki kuonekana kwamba yeye ni mtu wa aina fulani, kile unacho waza kinajidhihirisha katika mwenendo wako wa kila siku. Mtu fulani ,yawezekana ni mchumba wako au mwenzi wako ni rahisi kukujua ulivyo ndani ya moyo wako. Fanya tofauti ili watu wakufahamu msaada wako katika jamii unayoishi, kama nilivyo sema katika kichwa cha habari , hizi ni tabia zinazo fanana kati ya tabia nzuri na mbaya. 

Tabia mbaya au nzuri ina hatari ya kuongezeka kidogo kidogo na kukua kwa nguvu katika maisha, na kuacha inakuwa na shida au kuendelea nayo na kukupatia sifa njema katika jamii. kama wewe ni mvutaji wa bangi tabia hii itakua kila siku na kuwa sugu katika maisha, kama labda ni mtu unayependa kusoma neno la Mungu, tabia hiyo inaweza kukuwa sana na ukawa mtu wa mafanikio katia jumuia yako, watu watafanya maamuzi ya kuwa nawe au la. Anza kufanya majaribio ya kuwa na tabia njema utashangaa inakuwa na kukuwa kuwa kubwa sana na kila mtu atakuita heri katika dunia hii.

Tabia njema au mbaya ina leta faida kwa mtu mwenyewe au inaleta furaha, inakufanya ufurahie kadri inavyo kuwa sehemu ya maisha yako, yawezekana kabisa unapenda ngono, mahusiano yasiyo salama kati ya jinsia ya kike na ya kiume, kwa sasa imefikia watu wa jinsia moja kuwa na mahusiano ya ngono, hii siyo ajabu , wa kristo wanasema kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa, Watu wengi leo wameamua kutenda kunyume na Mungu na hii ndiyo inaitwa dhambi, kwa kweli ukianza tabia yeyote huwa inaleta furaha , mtu ataifurahia sana lakini mwisho wake ni maangamizi,. Endapo utaamua kufurahia kuwa mtu wa kujifunza neno la Mungu utajikuta unafuraha sana katika maisha  na utagundua kwamba Mungu anakubariki sana.
 Tutaendelea...



0 comments:

Post a Comment