Imeandaliwa na
Mchungaji
Lupakisyo Mwakobela Mwakasweswe
Simu ya mkononi: +255- 0764 150 391
Blogi:
Mwakasweswe.blogspot.com
Utangulizi
Katika fundisho hili tutajifunza
malezi bora ya watoto katika nyumba za watu wanamwamini Mungu. Ni wakati ambapo
wazazi wengi wamekata tama ya mazi ya watoto wao. Kumekuwa na changamoto nyingi
kwa jinsi yakuwa lea watoto wanaoishi katika kizazi chetu. Imekuwa kwamba
watoto nao wamejifunza na kuiga tabia ambazo wazazi wanashangaa kwamba wametoa
wapi? Limekuwa gumzo kanisani kwenye anyumba ya ibada , barabarani , katika
taasisi mbalimbali mjadala ukiwa ni jinsi gani watoto wasikuhizi walivyo na
tabia za ajabu .
Kwa kuzingatia umuhimu wa ujenzi wa tabia mwandishi na mjumbe wa Mungu anaandika katika
kitabu cha Elimu ya kikiristo uk 165
anasema “ Ujenzi wa tabia ni kazi ya muhimu kuliko zote alizopewa mwanadamu; na
kamwe kabla umuhimu wa kujifunza kanuni kwa makini haujakuwapo kama ulivyo
sasa.”
Katika somo hili tutajifunza mpango wa Mungu
kwa uzazi wa watoto, pia tutajifunza na
kuona wapi tumefanya makosa kama wazazi katika ujenzi wa tabia za watoto wetu.
Malezi ya watoto hayakosi changamoto
ambazo wazazi wanakutana nazo, yaweza kuwa kupitia maisha na tabia
walizojifunza kutoka kwa marafiki yaani makundi au kwa kuzipata kupitia malezi
ya wazazi wao. Changamot hizi ni pamoja na watoto kujiingiza katika unywaji wa
pombe, kuacha maisha ya ibada, kuvuta sigara na bangi, kuwa na mahusiano ya kingono
kati ya jinsia mbili na jinsia moja yaani ushoga, kutopenda masomo, kuwa na
ujauzito usio halali, magonjwa ya zinaa na Ukimwi.
Somo hili halitajadili maendeleo ya
mtoto katika ukuaji wake bali
litazungumzia malezi bora ya ujumla kwa watoto. Ni tumaini langu kwamba
baada ya somo hili, kila Mzazi atajua wajibu wake kwa malezi bora ya watoto
wake, kila mzazi atahisi mahali alipo fanya vibaya katika malezi ya watoto wake
pia atafanya yampasayo kutenda ili kuwa
na malezi bora ya watoto wake.
Mpango wa Mungu kwa wazazi; Adamu na Hawa
Mwanzo 1:27,28 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano
wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. 28 Mungu
akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na
kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe
chenye uhai kiendacho juu ya nchi. Mpango wa Mungu ulikuwa kumuumba mwanadamu kwa mfano wake, na
kwa maana hiyo mwanamke na mwanaume ni
mfanao wa Mungu.
Unaweza kujiuliza kwamba Mungu anafanana na mwanamke au mwanaume,
hilo si swala la kujadili kwani Mngu anaumba mtu kwa namna yake ya asili.
Mwanadamu ameumbwa akiwa mkamilifu katika njia zake mpaka pale dhambi ilipo
ingia na kumfanya mwanadamu apoteze sura ya ukamilifu wa Mungu.
Mungu
alifahamu kwamba hawa wazazi wangekuwa mfano bora katika maisha yao mbele ya
watoto wao, watoto wasingehangaika kuyafamu yaliyo mapenzi ya Mungu. Tunayo
furaha kwamba baada ya anguko la mwanadamu Mungu alifanya mpango wa ukombozi,
Yesu kristo akaja akafa badala ya mwanadamu, mwanadamu akahesabiwa kwamba ana
haki kwanjia ya Yesu kristo. Yohana 3:16
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee,
ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.Wazazi wanaqodumu
kuwa waaminifu wameahidiwa kuto potea bali wamehakikishiwa uzima wa milele.
Katika kitabu cha mwanzo 1:27, 28
Mungu akawabarikia wazazi wetu wa
kwanza, Mungu akawapa wajibu wazazi wetu wa kwanza , wazazi hawa alipewa kila
kitu kilcho kuwa muhimu kwa maisha yao. Mungu anajuwa kilicho muhimu katika
maisha yetu pia, aliweza kuwapatia wazazi hawa vitu maalumu vya kula hata vya
kutunza tu, kisha baada ya kuwabarikia, biblia inasema Mungu akawaambia, Zaeni .
Kuzaa ni agizo la Mungu tangu katika
bustani ya edeni, kuzaa ni agizo baada ya kubarikiwa, unaweza kugundua kwamba
Mungu hakutoa agizo la kuzaa mpaka kwanza alipo wabariki wazazi wetu, Mungu
aliwapa vitu muhimu vizuri vya kuwa navyo kabla ya kuzaa. Mungu wetu ni Mungu
wa utaratibu, hachanganyi mambo kama ambavyo mwanadamu anachanganya mambo, hebu
angalia, mzazi anajikuta ni mjamzito bila kujua nini cha kumpatia motto
anayetarajiwa kuzaliwa.
Siyo ajabu wazazi wengi wameanza
maisha bila kuju kwamba Mungu amewabariki kwa kuwa na vitu vya kuanzia maisha
hasa watoto wanapo anza kuja duniani, hebu fikiri mzazi, Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, zaeni. Je kabla ya kuzaa
ulijiandaa kiasi gani kuhusu maisha ya motto au watoto wako? Mungu hatoi agizo
la kuzaa kabla ya kukubariki.
Wazazi wengi wameiga kutoka kwa
wazazi wengine na kusema kila motto huja na bahati yake, hili limesababisha
watoto wengi wamezaliwa katika mazingira ya hatari sana, wengi hawajakutana na
nepi kama wengine wengine wamektana na vipande vya kanga nk. Agizo la Mungu ni
kubariki na kutoa agizo la kuzaa. Agizo la kubariki tumbo la uzazi liko
palepale lakini hakuagiza uzazi usio na mpango. Mungu anapoagiza, Mkaongezeke , alimaanisha vizazi na
vizazi na kuongezeka kwa namba ya wanafamilia yako nay a jirani yako, pia
alimaanisha Kujaza nchi, Mungu
anapendezwa na watu wanoweza kumwabudu kumsifu. Mungu alijua watu wengi
watakuwepo ambao watatangaza habari zake katika ulimwengu huu. Mimi na wewe
mzazi ni matokeo ya ongezeko la watu duniani.
Kwa taarifa ya sensa ya mwaka 2012 Watanzania tumefikia idadi ya watu 42,000,000( milioni arubaini na mbili) ongezeko
hilo ni changamoto kwa serikali na kwa familia, kwani linatakiwa ongeko la
miundo mbinu, chakula, maji, barabara , makazi mazuri , mpango mzuri wa uzazi,
Magonjwa ya wakina mama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano nk.
Agizo la Mungu kwa wazazi wetu wa kwanza ,waliambiwa waweze kuitiisha nchi Mwanzo
1:28 na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na
ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi. Wajibu
huu mkubwa wa kutiisha ni wajibu wa kila mzazi, kuhakikisha kwamba vinatii maagizo
yako, kutawala na kuhakikisha kila kiumbe kiendacho juu ya nchi kinatawaliwa
nawe, si ajabu ukashangaa kwamba viumbe wengine ambao bado hawajazaliwa utakuwa
na wajibu wa kuhakisha maisha yao yanatunzwa vizuri na wewe, zaidi sana wewe
kama mzazi ndiye unaweza kutiisha hata ujauzito ukatungwa kipindi utakacho
panga, kumbe kama mzazi utakuwa tayari kuendelea kumpatia elimu ya Mungu mtoto
wako uliye mzaa.
Bahati
mbaya wazazi wengi tumewaleta watoto duniani bila utaratibu na kujenga hoja
kwamba bado nina nguvu za uzazi na mayai bado yapo, hilo ni sahihi kabisa
lakini tukasahau kwamba Mungu wetu ni wa utaratibu, anabariki kwanza na anatoa
agizo kwamba Zaeni. Unaweza kupita
mitaani na usishangazwe na majina ya watoto kama vile Sikujua, Mapenzi , Yote haya ni kujipa matumaini kwamba Mungu
alipanga mtoto huyu azaliwe pasipo kujua, na wakati mwingine tumeseam ni
mapenzi ya Mungu, yote hayo ni sawa lakini tiukumbuke kwamba Mungu ni Mungu wa
utaratibu.
Ninajaribiwa kuamini kwamba ilipo fika wakati wa kugawa mali kwa
wtoto, wazazi wetu wa kwanza hawakupata tabu kwa sababu kila kilicho kuwa
hitaji la mtoto lilifanyika. Mwanzo 4:2
Akaongeza akamzaa ndugu yake, Habili.
Habili alikuwa mchunga kondoo, na Kaini alikuwa mkulima ardhi. Hebu
chunguza hapa kwa makini, Baada ya wazazi wetu kuongeza motto , Habili alikuwa
mtaalamu wa mifugo na Kaini alikuwa mtaalamu wa Shamba. Wazazi hawa walipoombwa
mali Ninaamini walitoa kwa moyo wote, Habili walimpatia kondoo za kumtosha , na
kaini walimpatia eneo kumbwa la ardhi.
Watoto ulionao na unaopanga kuwaleta duniani wanacho kitu cha kuwatosha kutoka kwako? Umebarikiwa kiasi gani
kuweza kuwaridhisha watoto wako. Unauelewa kiasi gani wa neno la Mungu kama
mafundisho awali kwa watoto wako, umejiandaa kiasi gani kwa malipo ya ada ya
shule na vyuo, unamaandalizi kiasi gani ya Vyakula katika nyumba yako.
Mungu wetu anautaratibu
mzuri. Tambua mbaraka wako kabla ya
kuzaa. Mwandishi E.white akieleza habari hii anasema “Wako wazazi
ambao, bila kufikiri kama waweza kuwatendea ipasavyo jamaa kubwa ama
sivyo, huzijaza nyumba zao watoto hawa wadogo wasioweza kujisaidia wenyewe,
wenye kuwategemea tu wazazi wao kwa matunzo na kwa mafundisho. Hili ni kosa
kubwa baya, si kwa mama tu, bali kwa watoto wake na kwa jamii ya watu mtaani.
Mtoto mikononi mwa mama mwaka kwa mwaka ni udhalimu mkuu kwake. Hupunguza , na
mara nyingi huharibu starehe na kuongeza uchovu wa kazi nyumbani.
Huwanyang’anya watoto matunzo, elimu na furaha amoto ulimwenguni ambayo wazazi
wangeiona kuwa ni wajibu wao kuwapa
(Wazazi) wangefikiri kwa makini riziki wawezazo kuwapatia watoto wao.
Hawana haki kuzaa watoto ulimwenguni kuwa mzigo kwa wengine”. AH
159 - 164
Wazazi wengi wamejikuta wakiwatukana watoto wanapohitaji mambo
muhimu ya shule. Nilishuhudia mzazi mmoja akiombwa na motto wake penseli ya
kuandikia shuleni naye akamjibu kwamba “wewe unadhani si tunakunya hiyo
penseli”. Niliamua kunyamaza ila niliumia sana, je motto amliumia kiasi gani?
Unadhani mapenzi ya mtoto huyo kwa mzazi wake huyo yakoje sasa.
Wazazi wengi wamepandikiza tabia mbaya kwa wtoto wao kwa jinsi
walivyo walea katika maisha yao ya utoto. Watoto wengi walijibiwa vibaya na
kupigwa kwa sababu ya wazazi kukosa vitu au mali kwaajili ya kusaidia elimu ya watoto
wao. Mungu anampango mzuri kwako wewe unayaendelea kuzaaa au unaye anza kuzaa,
Panga uzazi wako maana Mungu anabariki kwanza ndipo anaagiza mwanadamu azae
Malezi bora yanaendana na
mpango mzima wa maandalizi ya ujauzito na kuendelea kulea katika njia njema.
Tabia njema zitafundishwa kwa watoto endapo mzazi utafahamu maendeleo ya tabia
za watoto kutokana na mazingira ya kurithi na katika mazingira.
Malezi na Tabia za watoto kwa kurithi
Kumekuwa na changamoto kubwa sana kwa
wazazi katika kurekebisha tabia za watoto wao ambazo ni matokeo ya kurithi.
Watoto wengi wamezaliwa na tabia za wazazi wao au babu zao , kwa mfano hali za
moyo, akili, tabia za maumbile ya nje
kwa mfano rangi za macho na ngozi, mfumo wa meno, urefu, uzito, pamoja
na mihemuko.
Mara zingine motto anaweza kuwa hajiwezi
darasani ,hii inaweza kuwa sehemu ya kurithi, hii yaweza kusababishwa na mambo
mengi ambayo yanahusiana tangu utungaji wa mimba na malezi baada ya hapo.
Maandishi ya liyovuviwa yanasema “ Ikiwa
kabla ya kuzaliwa mtoto wake, mama mwenyewe ni mfisadi, kama ni mchoyo, mwenye
harara na mkali, tabia hizi zitaonekana kwa mototo . Hivyo watoto wengi wamerithi maelekeo mabaya wasiyoweza
kuyashinda ila kwa shida sana “AH 255 -267
Kwa namna nyingine , mzazi
asingeharakisha kutoa adhabu kwa motto wake kabla ya kukaa na motto wake na
kumweleza makosa yake. Mara zote isinge kuwa bora kuadhibu bila kujua kwamba
ulifundisha jambo unalolichukia kwa motto wako, endapo amejifunza kutoka nje
yako, pia ni vyema ukajiridhisha na kujua jinsi ya kuongea naye. Maandishi ya
uvuvio yanasema “ Akili za watoto ni nyepesi, nao hutofautisha sauti za uvumilivu,
na upendo na amri kali ya hasira, ambayo hukausha upendo na nia njema mioyoni
mwa watoto. Mama Mkristo wa kweli hatawafukuza watoto wake machoni pake kwa
ukali wake na kukosa huruma. “AH 232
-254
Malezi Na Tabia za watoto kutokana Na Mazingira
Sababu za Maombi
katika Familia
Kama
kuna jambo la muhimu katika familiani suala la ujenzi wa tabia watoto kwa
kupitia Nen la Mungu. Mithali 22:6 Mlee mtoto katika njia
impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mze. Kumbukumbu la Torati 6:7 nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na
kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na
uondokapo.Kumbukumbu la Torati 11:19 Nayo wafunzeni vijana vyenu kwa
kuyazungumza uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na
uondokapo.
Wazazwote wangefuata mashauri haya , watoto wengi wangaliweza kuwa
na maisha bora, lakini hujachelewa ” Baba na mama, kila siku asubuhi na jioni
wakusanyeni watoto wenu karibu nanyi,
kwa maombi ya unyenyekevu, inueni mioyo yenu kwa Mungu mpate msaada.” 7T 32-44
Sababu za kiuchumi
Wazazi wengi
wamekuwa wakijishughulisha na maswala ya kiuchumi ili kukidhi mahitaji ya
watoto wao. Imekuwa kwamba wazazi wengi wameshughulika lakini matokeo yake
yamekuwa hafifu hata kushindwa kutosheleza mahitaji ya watoto wao. Hii
yawezekana kwa kukusa kujituma (uvivu) kutokuwa na maarifa ya kubuni njia za
kupata fedha za kutunza familia zao.
Taifa la Tanzanai akwa ujumla
limekuwa likisisitiza kuhusu elimu ya ujasilia mali ambayao inamfanya mtu kuwa
mbunifu na kuanza kufanya kitu , kwa uchache sana wengi wamepuuza elimu hii na
wamebaki wakiwa na sababu za kutokuwa na mali za kulea watoto wao, hii ni
makosa kwa mzazi.
Sababu za
kiuchumi zinahusisha ni kwa jinsi gani mzazi umefanikiwa kuwa na kipato chako
binafsi, kuwa na uwekezaji, utunzaji wa fedha kwa ajili ya matumizi ya
baadaye,kuwa na madeni ambayo yamesumbua familia nyingi hata kukosa mahitaji
muhimu, kukosa katika hili kumewafanya wazazi wengi kukusa vitu muhimu yaani
chakula bora, afya nzuri ambavyo ni muhimu sana kwa ukuaji wa mototo.
Maandishi ya
uvuvio yanaeleza kwamba “Watu wengi walio maskini ni maskini kwa sababu hutumia
fedha zao mara tu wazipatapo” AH 392
Akiendelea anasema “Wale
wanajidai Kwa hali yoyote kuwa wenye utauwa, yawapasa kujivika mafundisho wanayo
yakiri, wala wasitoe nafasi kwa neon la Mungu hutukanwa kwa sababu ya mwenendo
wao wa kutojali. Mtume anasema, “ Msiwiwe na mtu cho chote” 5T179 – 182
Sababu za mlo
Sababu za kukosa chakula chenye viini
lishe, wazazi wengi wamejikuta watoto wao wakiwa na tabia tofauti katika makuzi
yao. Kukosa mlo kamili ni kosa kubwa katika malezi ya watoto. Hata Tanzania ,
tumebarikiwa kuwa na chakula cha mboga matunda ,nafaka, vyakula ambayo kama vingetumiwa vizuri vingeweza kusaidia
katika makuzi ya watoto na ujenzi wa tabia njema. Magonjwa mengi kama vile
kuishiwa damu , utapiamlo , na magonjwa mengine vimechangia sana katika
maendeleo mabaya ya ukuaji wa akili za
watoto.
Tabia za watoto wengi zimeharibiwa na jinsi
walivyp lelewa na kwa jinsi walivyo achwa hivyo , leo tunaweza kushuhudia
watoto wengi hata watu wazima wakifanya mambo tofauti kwa sababu tu ubongo wao
haukuandaliwa vizuri katik aumri wao mdogo.
Sababu za Magonjwa
na kuugua
Watoto wengi wameathirika akili zao Kwa kuwa na magonjwa ambayo
yameathiri akili zao, mihemuko yao na makuzi ya kijamii. Magonjwa Kama ya
mifupa, baridi yabisi, kuwa na usumbufu wa kutosikia vizuri. Yote haya
yanasababisha tabia za watoto ziwe tofauti na makusudio ya mzazi.
Inapasa wazazi kuwa makini katika kujikinga na
magonjwa mbalimbali yanayoweza kunyemelea watoto wako. Wazazi wengi wamepuuzia
kuwapeleka watoto wao katika hosipitali, kumekuwa na matangazo mengi ya
kupeleka watoto kwenye chanjo lakini ni wachache wanao itikia mwito huu. Hebu
kila mzazi atambue wajibu wake.
Sababu za Mazoezi ya
Viungo
Mazoezi ya
viungo ni dawa nzuri Kwa afya yakila mtu. Watoto wanafaidika Sana kwani mazoezi
yanasaidia kupunguza msongo wa maisha, yanasidia katika kujiamini, kuosa
mazoezi kumefanya watoto wengi kudumaa, wamejikuta afya zao zikiwa mbaya,
wameshindwa kukuwa kwa ulinganifu uliobora.
Katika eneo
hili, tamaduni zimechangia kutengeneza tabia za watoto, kwa mfano jamii nyingi
zimekuwa na ubaguzi wa jinsia.
Kwamba watoto wakiume wamechukua sehemu ya juu
sana na kuonekana wanafaida kubwa katika jamii kuliko wana wa kike. Watoto
wengi wa kiume wamekuwa wakishindwa kufanya kazi ndogo za nyumbani kwa
kutegemea kuwapo kwa wasichana. Watoto w kike wameshindwa kupata elimu
kwasababu wazazi wengi wanadhani watoto wa kike ni wa kuolewa tu. Maandiko
matakatifu katika kitabu cha Mathayo 25:40 Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin,
nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea
mimi. Swali kubwa Kwa wazazi leo, tunawafundishaje watoto wetu katika mila na
desturi zetu? Tabia zao zinaathirika kwa kiasi gani? Yesu anasema kwa kutenda
kwetu.
Hii imefanya tabia za baadhi ya watoto wa kike
kutojiamini katika maisha yao na kujiona kwamba wao ni wa kuolewa tu hivyo
huanza tabia za kutafuta kuolewa hata kabla ya umri unafaa. Wazazi wangejifunza
kwamba Mungu hana Upendeleo wala ubaguzi. Kwa kufanya hivi ni kumkosea Mungu.
Tamaduni hizi zimekumba nyumba za
ibada. Wazazi walio wafundisha watoto wao kwamba wao hawafai kusimama mbele za
wana wa kiume mpaka sasa wamekuwa na tabia ya woga, wa meshindwa kushiriki
kikamilifu katika kazi za kanisa na shughuli mbalimbali za mahali pa ibada ya
Mungu. Tabia hizi ni matokeo mabaya ya kuwa na tamaduni ambazo hazina ukubali
wa maandiko matakatifu ya Mungu kwani Mungu alipoumba mwanadamu alitaka kila
mtu amwabudu yeye.
Maandiko matakatifu katika kitabu cha
Ufunuo wa Yohana 14:7
akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu
yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na
chemchemi za maji
Hakuna
aliyeachwa katika kusujudu mbele za Mungu, hakuna aliyeachwa katika kumcha
Mungu na kumtukuza kwa sababau hukumu italetwa kwa kila mtu, haijalishi ni
jinsia ya kike au ya kiume, hivyo basi tamaduni mila na desturi zisifanye
wazazi wengi kuwafundisha watoto tabia zitakazo haribu maisha na wokovu wao.
Changamoto za malezi ya watoto katika kizazi hiki
Unywaji wa pombe ,Katika ulimwengu huu wa
sayansi na technolgia, kuacha maisha ya ibada, Uvutaji wa sigara, bangi,(
madawa ya kulevya) kuwa na mahusiano ya kingono kati ya jinsia mbili na jinsia
moja yaani ushoga, kuwa mtoro wamasomo, kuwa na ujauzito usio halali na kupata Magonjwa
ya zinaa na Ukimwi.
Pamoja na changamoto hizi, mzazi
anapaswa kumwombea motto wake ili kwamba Mungu aepushe balaa hizi. Wakati
Fulani unaweza ukapatwa na majaribu kwamba mtot wako amejiingiza katika moja
wapo ya hayo, kumbuka endapo ulimkabidhi mikononi mwa Mungu, Mungu bado
anazungumza pamoja naye maana hata acha mafundisho aliyopewa na mzazi hata
atakapo kuwa mzee. Endelea kuomba na akuomba na kuomba.