UTANGULIZI
Muasisi Mkuu wa Muziki na Uimbaji ni
Mungu. Muziki uliumbwa kwa matumizi
matakatifu, kuinua mawazo kwa mambo yaliyo safi, mema na kuamusha katika moyo
ibada na Shukurani kwa Mungu.” Ellen
White anaendelea kusema: “Muziki ni moja ya sanaa ya pekee. Muziki mzuri hauleti tu burudiko la rohoni,
bali pia bali huyainua akili katika vimo vya juu kwa mambo mazuri. Mungu mara nyingi ametumia nyimbo za kiroho
kugusa mioyo ya wadhambi na kuwaongoza kutubu. Kwa upande mwingine nyimbo
zaweza kubomoa tabia adilifu na kututenga mbali na mahusiano yetu na Mungu.”
Mama Ellen katika toleo hilo lililotajwa hapo
juu ana haya ya ziada kuhusiana na kitengo ch a Muziki¨ Ellen G. White, Tumaini
la Vizazi Vyote. Washington DC: Review
and Herald Publication Association p 73 Ibid., Uinjilisti wa Vitabu uk 43 Muziki waweza kuwa
na mvuto mkumbwa kwa ajili ya mambo ya kupendeza, hata hivyo Hatujatumia huduma
hii katika ibada kama ipasavyo. Mara nyingi nyimbo zimeimbwa Kiholela bila mpangilio maalumu kufuatia
matukio Fulani na mara nyingi wale wafanyao. Huduma hii wameachwa kufanya
wapendavyo, na hivyo muziki hupoteza makusudi yake Kwa wale wanaosikiliza. Muziki ni muhimu kuwa na Uzuri, mvuto na
nguvu. Hebu sauti Ziinuliwe kwa nyimbo
za sifa na ibada. Utumiaji wa vyombo waweza kushirikishwa ili Utamu wake
umfikie Muumbaji kama sadaka inayokubalika.” Ibid., uk 114
Muziki ulibuniwa na Mungui kwa ajili ya Ibada,
Ukaagizwa na Mungu na , Ukabarikiwa na Mungu.
Wakati wa uumbaji nyota za asubuhi ziliimba na kwaya ya malaika wakapaza
sauti zao kwa furaha. (Ayubu
34:4-7). Sehemu inayofuata tutaona jinsi
Muziki ulivyovurugwa na adui.
HISTORIA YA ANGUKO AU UCHEPUKAJI WA VIWANGO
VYA MUZIKI
VITA KUU BAINA YA KRISTO NA SHETANI
KATIKA MUKTADHA WA MUZIKI
Vita kuu baina ya Kristo na Shetani ambayo
ilianzia kule mbinguni ikafanya Lucifer MalaikaAliyekuwa kiongozi Mkuu wa Kwaya
ya Malaika kule mbinguni alipotamani nafasi ya Mungu kama alivyotamka
“nitakipandisha kiti changu juu kupita nyota za Mungu….nitafanana kama Mungu”
Lucifa alitaka aabudiye. ( Isaya 14: 13,14 ) Mungu anataka aabudiwe na ndiyo
stahili Yake kwa maana yeye ndiye muumbaji wa wote. Shetani naye anataka aabudiwe
Na amefaulu Sana kupokea ibada ambayo
haimstahili kwa kupitia kuwakilisha tabia ya Mungu vibaya kwa njia ya Muziki
ambao ameuandika ili kusudi kulishinda kanisa la Mungu. Mdanganyifu mkuu
akitambua ya kuwa muda wake ni mfupi sana amebuni njia hii ya kuwanasa
Waadiventista Wanaodai kuwa wanamtii pamoja na kushika Sabato yake takatifu na
kutunza amri kumi za Mungu kwa kupitia Muziki wa duniani ambao haumpi Mungu
utukufu na Sifa badala yake humpa Ibilisi utukufu na Sifa japo unaimbiwa mbele
ya kusanyiko takatifu la wasafiri wa mbinguni.
Ibilisi akitambua kuwa
Ibada ndiyo njia rahisi ya kuliharibu kanisa la Mungu, amekusudia kuharibu
utakatifu wa Muziki katika Ibada kuanzia katika bustani y Edeni. Vita kuu ya
Muziki ambayo ilianzia katika bustani ya Edeni ni halisi, na hivyo ni muhimu
kwetu kuelewa kama kanisa jinsi ambavyo uimbaji umeharibiwa leo na Yule adui,
na sasa hebu na tufuatie historia ya Muziki na uchepukaji katika kanisa la
Mungu la kweli.
ANGUKO LA KWANZA CHINI
YA MLIMA SINAI
Historia inaanzia na
Waisrael wa Zamani (ambapo sisi tu Waisrael wa Kiroho). Wakati walipokuwa wakisafiri baada ya Mungu
kuwaokoa kutoka katika utumwa wa Misri
wakielekea katika nchi ya ahadi (Kaanani); wakati Musa alipoagizwa
kukwea mlimani ili kupokea amri kumi za Mungu, watu (wakiongozwa na Kuhani
Haruni) Walishangilia na kufanya ibada kwa ndama wa dhahabu, wakitoa sadaka,
wakinywa na kucheza na kuimba. Muziki ambao uliambatana na Sherehe yao ulikuwa
na Sauti kubwa na usio na mpangilio
kiasi ambacho Joshua alipokuwa akishuka toka mlimani pamoja na Musa
wadhani ya kuwa illkuwa kelele za vita.
Lakini Musa Mtumishi wa
Mungu akasema, La hasha; ni kelele za
watu wanaoimba. ( Kutoka 32:18). Jinsi watu walivyoimba na kucheza Haruni akawa
akawaongoza hata kubakia uchi wakimshangilia
ndama wa dhahabu, ibada ambayo iliwaangusha katika zinaa. ( Kutoka 18:25
). Huu ulikuwa uasi wa Kwanza Mkuu kwa watu Wateule wa Mungu katika siku za
awali kabisa za kanisa la Mungu. Muziki huu ambao ulibuniwa na Shetani
ulikusudiwa kuwafanya watu kumvunjia Mungu heshima. Kama matokeo ya kumtii Yule
adui na kukengeuka katika njia ya Mungu “wakaanguka watu wasiopungua elfu
tatu.” (Kutoka 32:28)
ANGUKO LA PILI MASHARIKI MWA YORDANI
Takribani miaka kama
arobaini (40) baada ya kuvuka bahari ya Shamu, wakati Musa Mtumishi wa Bwana
alipokuwa tu amekwisha kutoa maagizo ya muhimu kabla ya kuvuka mto Yoridani ili
kuingia katika nchi ya ahadi waliengesha mahema yao Baali- Peori upande wa
mashariki ufuoni mwa mto Yoridani Watu
wa MUNGU kwa njia ya kujichanganya na mataifa wakaanguka katika anasa.
Kwa mara NYINGINE TENA walishiriki katika
Muziki wa mataifa na kucheza. Tendo hili likawapeleka mbali zaidi wakazama
katika anasa, unywaji na ibada ya sanamu na muziki ule ukawafanya wakaanguka
katika zinaa na kuanguka kiroho. Kwa njia hii Waisraeli walijiunga na ibada ya
kipagani na kumuasi Mungu. Na kwa mara
nyingine tena adhabu kubwa iliwaangukia na zaidi ya watu elfu kumi
waliangamizwa. Ibid. Wazee na Manabii 453-456
BAAL – PEORI YA KARNE YA LEO
Leo watu wa MUNGU kwa
mara nyingine tena Waadiventista wa Sabato tupo tumepumzika katika mipaka ya
Kaanani – Kaanani ya Mbinguni. Swali la Kujiuliza ni hili Je inawezekana kuona
hali ile ya uasi kama ilivyokuwa katika Baal- Peori katika makanisa yetu ya sasa? JIBU
NI NDIO
Tupo katika kingo za
Yordani tayari kwa kuingia katika
Kaanani ya Mbinguni ila tunachelewa hapo wakati tunangojea kumwagwa kwa Mvua ya
Masika, na Kutoa kilio Kikuu cha kuutangaza ujio wa mwokozi wa haraka. Swali
jingine la kujiuliza ni hili je wengi wetu makanisani hatujafanana na madhehebu
mengine hasa katika suala la ibada kwa
njia y Muziki? JIBU LA SWALI HILI PIA LAWEZA PIA KUWA NDIO. Angalizo letu n ( 1 Yohana 2 :15)
ANGUKO NAMBA TATU ( 3 ) MARA TU BAADA YA
MWAKA 1844
Baada ya tukio la Baal –
Peori tunaposafiri kihistoria tunaingia wakati ambapo kanisa hili lilikuwa
changa ndipo tu limeanza baada ya Mwaka 1844. Baada tu ya Mwaka 1844 wakati
waumini watangulizi walipokuwa wanatazamia ujio wa Kristo kwa mara ya pili na
kukosa kuja,
Kama vile inavyoweza
fananishwa na Waisrael walipoanza safari yao ya kuingia katika kaanani ya
duniani; watangulizi wenzetu walianza safari yao ya kuelekea katika kaanani ya
mbinguni. Katika kipindi hicho kulikuwa
na hali Fulani ya utata katika historia ya Muziki wa Kiadiventista. Ellen White anaeleza juu ya ekengeukaji
uliojitokeza mnamo kipindi hicho kule Marekani. Katika sehemu nyingi Muziki
wetu uliingiwa na hali ya makelele, kuruka na kucheza. Mjumbe wa Mungu alitumwa na kusema yafuatayo:
“ Nilitoa ushuhuda wangu kama onyo katika jina la Bwana nikikemea hali hii
iliyojitokeza.” Jambo la kutisha ni
kuwa katika tukio hili baada tu ya mwaka 1844, watu walikaa uchi na matokeo
yake yakawa kukengeuka na uovu ndio yalikuwa matokeo yake.
Ki historia ni muhimu kuelewa ya kwamba
kipindi hiki kanisa likiwa bado changa kuanzia mwaka ( 1865 – 1900 ) ndicho
kipindi cha ugunduzi wa Muziki wa Jazz na Jazz ni jina linalosimama badala ya
kujamiana (sexual intercourse ) ambalo lilichipuka katika nyumba za makahaba
kule New Orleans, Lousiana . Hiki ni
kipindi ambacho marekani ilisumbuliwa na nyimbo hizi ambazo zilikuwa mpya na
zikiwa na alama ukosefu wa adabu na kinyama pamoja na kuleta aibu.” Ibid., 2
Nyaraka Zilizochaguliwa (SM) uk 3 J.
Simons. Nyimbo za mporomoko wa Maadili,
uk 35-39
Angalizo hapa ni kuwa wakati kanisa la Mungu la kweli
lilipokuwa limeanzishwa na bado changa, Mwana muziki aliyeanguka alikuwa pale
tayari kuharibu utakatifu wa Muziki katika ibada ya kanisa ambalo analichukia
sana. Shetani anahitaji ibada yetu. Kwa
kuanza kuandika Muziki mpotovu ambao pole pole ungelitoa kanisa katika njia
yake sahihi na kuleteleza ujumbe wa malaika wa watatu.
Angalizo jingine ni
kuwa Shetani ambaye ni Mwana Muziki Mkuu aliyeongoza kwaya ya malaika watakatifu kule mbinguni,
amegundua kile ambacho ana uwezo wa kukishambulia katika maisha ya mfuasi wa
kristo nacho ni kutawala na ubongo wa binadamu kwani ni kwa njia hii ambayo
Mungu anatumia kuwasiliana na binaadamu”
Iwapo ubongo wa binaadamu ndio unaotawala maisha
ya binaadamu hivyo basi kuna mantiki kwamba Shetani atafanya shambulizi lake la
kwanza na la Mwisho kwa njia ya kutawala ubongo wa binadamu. Na iwapo Muziki ni
zana ya muhimu sana katika matashi na tabia ya mwanadamu hivyo itakuwa kawaida
kueleweka kuwa, Shetani atatumia Muziki kufikia malengo yake ya kumshambulia
mfuasi wa kristo Ibid. uk 352
ANGUKO LA MSINGI WA MUZIKI SEHEMU YA NNE (4)
KATIKA JIMBO LA INDIANA (MAREKANI)
Katika Konferensi ya
Indiana kule Marekani mnamo mwaka 1900 lilitokea tukio jingine Ambalo lilikuwa
la kutisha katika kanisa letu. Baadhi ya Makanisa yetu kule Indiana yalikuwa
yakiendesha ibada zikiwa na nyimbo zenye moto wa kigeni.
Nyimbo hizo zilisikika
katika sauti kubwa , zikiwamo ngoma , sauti nzito za vyuma na ghasia zingine.
Muziki tena ulio na mchanganyiko wa kishetani ulidhihirishwa katitka makanisa
hayo na Roho mtakatifu kwa kawaida asinge tamalaki katika ibada kama ile
alisema mjumbe wa Mungu, Ellen G. White. Kufuatia tukio hili la Indiana , Ellen
G. White alitabiri ya kuwa hali hii ya Muziki uliojaa makelele na ukiwa na
dalili zote za kishetani katika ibada,utaletwa tena katika kanisa la
Waadiventista wa Sabato muda mfupi tu kabla ya kufungwa kwa mlango wa
rehema.”Sikiliza vile mjumbe wa Mungu asemavyo kufuatia tukio lile kule
Indiana: Ibid ., uk 36
“mambo uliyoelezea
kutokea kule Indiana, Mungu amenionyesha kuwa Yatarudiwa tena kitambo kidogo
kabla ya kufungwa kwa mlango wa rehema.
Kila aina ya vitu visivyofaa vitaachiliwa. Kutakuwepo na makelele,
upigaji wa Ngoma kuimba na kucheza. Via vya kufanyia maamuzi vitapumbazwa kiasi
Kwamba haviwezi kuaminiwa kufanya uamuzi ulio sahihi na hii itaitwa ni Huduma
ya Roho Mtakatifu wa Mungu. Roho Mtakatifu kamwe hawezi Kujidhihirisha kwa njia
hii, wala katika sauti za makele kama zile. Hizi ni Mbinu za shetani za kutweza ukweli. Ni bora
kutokuwa na muziki wa jinsi Hii wa kumsifu Mungu kuliko kutumia muziki na jinsi
hii ambao mweziJanuary nilijulishwa kuwa muziki huu utaletwa katika mkutano wa
Makambi. Ibid. 36
JE KUCHEZA DANSI, VITENDO NA KUMACHI NA
MIHEMKO VINA MWONEKANO GANI KATIKA HUDUMA YA UIMBAJI?
Swali la msingi ni hili
je kucheza wakati wa uimbaji ni sahihi? (Shall we dance?) Jiibu la swali hili
laweza kutokana na kile ambacho kimekwisha onekana katika historia ya Anguko na
ukengeukaji wa Muziki kuanzia Edeni, Chini ya mlima Sinai, Baal – Peori mahali
Waisrael walipojenga hema hali wakijiandaa kuingia Kanani. Pia walipokuwa
wakivuka Bahari ya shamu, Katika Mikutano ya Makambi kule Indiana, Baada ya
mwaka 1844, na miaka ya 1990 na kuendelea ambapo imekwisha bainika kuwa
Walisrael walipokengeuka katika
kujichanganya na mataifa, kushiriki katika sherehe zao, za ulafi, makelele ,
kuruka na kucheza kuwa adhabu yake ilikuwa kumbwa na hivyo Mungu hakupendezwa
na mtindo wa jinsi hiyo wa ibada. Hivyo basi kucheza dansi hakukubaliki katika
ibada takatifu.
Ni muhimu pia kupata
ushauri mwingne toka kwenye Biblia juu ya suala hili. Mara nyingi kitendo cha
Mfalme Daudi kinatafsiriwa visivyo.
Maandiko ni kweli yanashuhudia kwa maneno yafuatayo: “ Naye Mfalme Daudi
akacheza mbele za Bwana kwa nguvu zake zote.”
Mfalme Daudi alicheza sio katika mazingira ya Ibada. Uchezaji wake
ulifanyika nje ya ibada ndani ya hekalu, na hiyo inaleta tofauti kubwa. Kucheza kwa Daudi kulifanyika katika
mazingira ya Sherehe ya kushangilia na kushereheka moyoni kwa kuona ya kuwa
hatimaye Sanduku la Agano la Bwana limerejeshwa Yerusalemu. ( 2 Sam 6:14, 16 ).
Hivyo basi hapa kuna
tukio tofauti na lile ya wakati ibada inapokuwa inaendeshwa katika hekalu. Miriam na wanawake walishika Makuyamba na
wakiimba na kushangilia ukuu wa Mungu wakati alipowavusha katika bahari ya
Shamu na kuwashinda Wamisri na jeshi lake walipogharakishwa ndani ya bahari ya
Shamu. ((Kutoka 15:1-21)
Wanawake waliimba na
kucheza wakati Daudi alipomshinda Goliath (I Sam 18:6,7 ) Binti wa Jephthah
aliimba na kucheza alipokuwa anampokea baba yake wakati akitoka vitani kuwaamua
waisrael toka kwa maadui zao. (Waamuzi 11:34). Hivyo twaona ya kuwa kucheza
dansi kusiwe na uhusiano wakati huduma ya nyimbo inapokuwa inafanyika katika
ibada takatifu.
Kufanya Vitendo,
Kumachi na Mihemko vinapunguza uzito wa ujumbe ambao umetolewa katika huduma ya
uimbaji kwani wasikilizaji badala ya kutafakari ujumbe unaotolewa badala yake
usikivu wao unagawanyika kuangalia usanii wa mihemko ya waimbaji, au Maching au
usanii wa vitendo hivi kwa kiasi kikubwa
vinahafifisha ujumbe wa mahubiri yanayotolewa na mhubiri wa Kwanza Yaani Kwaya.
Hivyo ili kuongeza usikivu wa wasikilizaji ni muhimu ya kuwa wahudumu.Waruhusu
ujumbe wao uende kama ulivyotolewa bila ya kuongeza vikorombezo vya vitendo vinavyofikiriwa
kuwa vya muhimu. Utukufu kwa Mungu
kusudi la Uimbaji
Kusudi
kubwa la huduma ya uimbaji nikwa ajili ya kumtukuza Mungu. Mwimbaji
anabadilishwa na wasikilizaji pia wanabadilishwa na ujumbe wanaousikia kupitia
wa kwaya. Mawazo yao, huzuni zao,
Masumbuko yao, misiba yao, mikasa ya maisha vyote vinakutana na ujumbe wenye
matumaini kwa Mungu ambaye kwa kumtumainia aweza kuwachukulia mizigo yao na
kuwaweka huru. Hii ndiyo sababu ni muhimu
ujumbe uende kama ulivyo ili mwishoni wasikilizaji wasije wakawatukuza wahudumu
kwa ajili ya matendo yanayoonekana kwa macho ya kibinaadamu badala ya kurudisha
utukufu kwa Mungu.
Muziki wa kiadiventista
unapaswa kuwa na tofauti na muziki unaotolewa na wahudumu wengine ambao sio
waadivenstista. Kwa vile Waadiventista
ni watu wa pekee kwa kila kitu. Muziki pia unapaswa uinue bendera ya
uadiventista na Kristo atukuzwe katika huduma zao.
MATUMIZI YA VYOMBO VYA MUZIKI KATIKA IBAD
Vyombo vya Muziki vyaweza kutumika katika Uimbaji iwapo mambo ya fuatayo
yatatiliwa maanani:
- Mpigaji wa vyombo kwa mfano Piano au
Kinanda ni budi awe mtaalamu wa kutumia vyombo hivyo.
- Mchezaji
awe na Ujuzi wa kusoma Notes na kucheza (Awe mjuzi wa Tonic so lfa na
Staff Notation.
- Mchezaji asitumie
miziki iliyoandaliwa na kuhifadhiwa katika Keyboard au Piano (Ready made
Musical accompaniments) Atawale Keyboard au piano au Organ badala ya
kutawaliwa na vyombo hivi.
- Aepuke Sana
matumizi ya sauti ya juu, midundo, ambayo inatisha na kuwafanya watoto
wadogo waogope.
- Ahakikishe
kuwa sauti ya vyombo hivyo, inaruhusu maneno yasikike (lyrics) ambayo
ndiyo hasa muhimu katika muziki.
- Awe
mnyenyekevu, awe tayari kupokea mashauri asiwe na kiburi ambacho ndicho
kilileta anguko la Mkurugenzi wa awali ya kwaya ya Mbinguni ambaye
hatimaye alianguka kwa sababu ya kiburi chake.
- Afahamu
jinsi ya kutawala sauti ya vyombo iende sambamba ikiacha nafasi ya maneno
kusikika vema (melody, harmony rhythm na balance. ) viende sawia.
- Awe
tayari kushirikiana na Uongozi wa Kanisa.
Angalizo: Iwapo vigezo hivyo havizingatiwi, ni bora kuimba
bila kutumia vyombo vya Muziki.
MAAMUZI YA MKUTANO ULIOFANYIKA KWAKOA (NETCO)
MWAKA 2003 CHINI YA IDARA YA VIJANA NA NYIMBO
Mnamo mwaka 2003 kule Kwakoa katika wilaya ya Mwanga, kamati iliyoteuliwa
na kupewa majukumu ya kushughulikia maswala ya Nyimbo hasa kuhusiana na
matumizi ya Vyombo vya Muziki (Accampaniments) Maamuzi yalikuwa kama ifuatavyo:
•
“Watumiaji wa
vyombo vya muziki hasa Vinanda ambao hawana ujuzi wa kitaalamu wa matumizi ya
vyombo hivyo, Waache kutumia katika kwaya vyombo hivyo hadi watakapokuwa na
wataalamu ambao wamejifunza Kusoma na Kucheza vyombo hivyo.Hivyo iliwekwa
bayana kuwa kutumia vyombo vya Muziki, Kinanda, au piano ndicho kiwango
kinachotakiwa. Matumizi ya beats au
midundo na mapigo vulivyopandikizwa katika Vinanda viachwe kabisa. “
•
Konferensi hii
chini ya uongozi wa Mchungaji Izungo wakati akiwa Mwenyekiti wa Konferensi
wakati huo. Alitoa msimamo ambao ni bora ufuatwe na kitivo cha Muziki cha
Kanisa.Unangalifu unahitajika kufanyika katika maeneo haya kwani hii ni sehemu
dhabiti ya Msukumo wa Kanisa la Waadiventista wa Sabato ulimwenguni ulio na
kauli mbiu ya “Uamsho na Matengenezo.” John Kimbute, Mwenye kiti wa Kamati ya Muziki
wa Konferensi, Kwakoa NETC, 2003.
Kwa Kuzingatia Maamuzi hayo ambayo kwa kiasi kikubwa yamebadilisha na kupunguza
kasi iliyokuwepo ya matumizi ya vyombo hivyo kiholela inapokuwa sio kwa
makanisa yote bali yapo matengenezo ambayo ni dhahiri. Kwa kuunga mkono maamuzi
hayo Samuele Bacciocchi katika kitabu chake kiitwacho: The Christian and
Rock Music, anayo haya ya kusema:
•
“Viongozi wa
Ibada wanaosisitiza utumiaji wa vyombo kadhaa, kama vile Ngoma, Magita yenye Sauti nzito ya Bass (Bass
Guitar) na magita yenye pandikizo la kutoa muziki wa “Rock” katika makanisa yao
wanapaswa waelewe ya kuwa kule Yerusalemu katika hekalu na katika hekalu
la mbinguni hakuna vyombo vya jinsi hiyo vinaruhusiwa.” Samuele Bacchiocchi et
al Tha Christian & Rock Music A
Study on Biblical Principles of Music. Michigan: Bilbical Perspective,2000) P
177
•
“Viongozi wa
Ibada wanaoruhusu waimbaji kutumia Ngoma,Magita ya Bass na Magita ya kuvuma sana ili kuleta sauti ya muziki
wa Jazz au rock ni muhimu kwao watambue
ya kuwa katika hekalu la Bwana kule Yerusalemu na pia katika hekalu la
Mbinguni. Hapakuwa na vyombo vyenye
sauti kubwa zinazotengeneza (Okestra) katika ibada. Kinyume chake vilikataliwa
vyombo aina mbili na vyote vya nyuzi tu ndivyo vilivyoruhusiwa kutumika katika
ibada” Ibid Ni vema pia ieleweke kuwa hakuna kosa lolote kutumia filimbi na
Matoazi. Ila vyombo Hivi havikutumiwa kwani vilikuwa vimezoeleka katika
matumizi ya miziki ya duniani(Secular Music )
.
•
Iwapo vyombo vya muziki vyenye sauti kali vingeruhusiwa
kutumika katika ibada, ibada ingebalishwa kuwa mahali pa maburudisho. Hata
wanawake Ambao walizoelea sana kucheza dansi hawakuruhusiwa kuwa sehemu ya
kwaya. Daudi alichagua wanaume kuwa tu ndio waimbaji. Hii haina maana kuwa wanawake leo
wasijumuishwe katika kwaya isipokuwa iwapo wapo ambao ni wachezaji dansi katika
miziki ya kidunia (dance) iwapo hao watafahamika, si vema wahusishwe katika
muziki wa kumsifu Mfalme wa utukufu. Hii
ina maana kuwa wale wanaocheza miziki ya kidunia kama kazi wasingeruhusiwa
kusimama mbele za mkutano wa watakatifu na kumtukuza Baba wa Utukufu. Hili ni
angalizo la muhimu.
NYIMBO ZA KIHOLELA
ZIMEHARIBU SURA YA MUZIKI
WA KIADIVENTISTA
Ili kurejesha sura
ya Muziki wa kiadiventista ni muhimu kwaya pamoja na vikundi vya kwaya
vizingatie machache yafuatayo:-
- Uimbaji upangwe katika Notes 1.
Tonic Sol fas na 2. Staff
Notation
- Nyimbo zisiimbwe bila mpangilio kujifunza kwa
muda wa kutosha ili zinapoimbwa ziwe zinasikika vizuri.(kwaya ya mfalme
Daudi ilifunzwa kwa mda wa miaka mitano)
- Ni vema Theme za Nyimbo zetu zizingatie Ujio wa Yesu, Huduma ya Kristo katika patakatifu na Sabato ambalo ni tarajio la pumziko la milele pale Mungu atakapofanya maskani yake pamoja na Wanaadamu.
- Kwaya au Vikundi vya Uimbaji viwe na sare
inayoelewekaKwani waimbaji ni
wahubiri.-sare ziwe mavazi ya heshima na kusitiri mwili
- T shirts zisitumike kama vazi la kusimama mbele
ya kusanyiko la watakatifu, na kila aina ya mavazi yanayoweza kuhafifisha
huduma ya ibada( isipokuwa katika matukio maalumu)
- Waimbishaji wawe na taaluma katika kuongoza
nyimbo wafanye bidii katika kujifunza namna ya kufuata mapigo.
- Kwaya na Vikundi vyote viandikishwe na
kupitishwa na kanisa mahaliaHebu tujifunze kwa kuangalia mfano wa kwaya za
mbinguni
MFANO WA MUZIKI WA KWAYA ZA MBINGUNI
Hebu na tujifunze katika kwaya tatu zilizoko mbinguni. Samuelle Bacchiocchi katika utafiti wake wa
Theolojia ya Muziki wa Waadiventista wa Sabato anatujuza kuwa kufuatana na
Utafiti wa Oscar Cullman katika kitabu cha Ufunuo kuna kwaya tatu kule
mbinguni:- Kwaya ya Wazee Ishirini na Nne (24 ) Ufunuo 4:10 – 11) Mada yao
kuu ni kumsifu Mungu kama Muumbaji Wakisema . Wewe Bwana ndiwe unastahili
utukufu, heshima na Uweza, na mwisho wanamsifu Mungu kwa ajili ya wale
waliokombolewa na sifa kwa mwana kondoo wa Mungu ( Wanaimba kutumia
Vinubi) harps). Yohana anasema,”
Nikasikia sauti kutoka mbinguni kama sauti ya maji mengi, kama sauti ya
Ngurumo ndipo nikasikia sauti toka kwa Wapiga vinubi wakipiga vinubi
vyao”( Ufunuo 14;2) Pia wanaimba wimbo mpya (Ufunuo 5:8-9)
Malaika na Waliokombolewa ambao hesabu yao ni kubwa. (Ufunuo 5:11-12; 7:9-12) Mada kuu ni sawa na ile ya Wazee ishirini na
Nne Kwaya ya Wote (Mass Choir)
ikihusisha viumbe wote na Waliokombolewa (Ufunuo 5:13) Wakiwa na matawi ya
mitende na mavazi meupe.Mada yao kuu ni: Wokovu ni wa Mungu wetu aketiye katika
kiti cha enzi na Mwana Kondoo.(Ufunuo 7: 9 – 10) Wote wanaelekeza sifa na Utukufu kwa Utatu
Mtakatifu.
Kufuatana na Thomas Seel anasema
kuwa Kinubi ambacho ni chombo cha nyuzi pekee kinachotumika katika kwaya za
mbinguni katika ibada kimepewa kibali kwani ni rahisi kuendana (blending) na
sauti za waimbaji.” IbidYohana wa Ufunuo
anatumia neno “Prokuneo” akiwa na maana ya kuwa muziki wa mwisho wa wakati ni
muhimu uonyeshe heshima na kicho ili sifa zielekezwe kwa yeye ambaye
anastahili,baba wa mbinguni.
HITIMISHO
Mambo makuu (5) ni ya
Muhimu kuzingatiwa katika huduma ya Muziki
- Muziki wa Kiadiventista ni muhimu uonyeshe
heshima na kicho mbele za mahali pa ibada kwani ndio wakati tunakutana na
Mungu
- Vyombo vya kuzindikiza Muziki vichezwe na
wataalamu wa kuvitumia vyombo hivyo na visisikike zaidi na kuzuia maneno
ambayo ndiyo yamebeba ujumbe wa Mungu.
- Muziki unapotolewa uonyeshe Furaha na
uchangamfu wa kuwa mbele za Mungu (Uf. 7:12)
- Uwiano uwepo katika Ujumbe unaotolewa na
mpangano wa Sauti na ulete somo mahususi linaloweza kueleweka
- Waimbaji
wa Kwaya ya Kanisa na Vikundi wawe na sare kadri iwezekanavyo na
mavazi ya heshima ya kujiwasilisha vizuri mbele ya watu na Mbele za Mfalme
wa Wafalme na Bwana wa Mabwana.
- Muziki na huduma ya Uimbaji katika maandiko ni
sawa kama Sadaka ya Shukrani kwa Mungu, Ya Uumbaji, ulinzi wa Mungu na Wokovu
wa Milele.
- Hebu tufanye matengenezo ya kuturejesha katika
mapito ya zamani wa Muziki wa Kiadiventista. (Yeremia 6:16.) Mungu na awabariki.
2 comments:
UBARIKIWE PR, HILI SOMO NI SOMO MWAFAKA SANA
Imekuwa Mbaraka mkubwa, naomba kama itakupendeza hizo nukuu hasa pale ulipoandika Ibid ingekuwa umeitaja kabisa maana ukisoma nukuu inayokuwa imetangulia kisha ukikutana na nukuu inayosema Ibid unakosa muunganiko wa hiyo nukuu hasa unapoenda katika kitabu rejea .
Unaweza kutuweka footnotes ambayo zitatuelekeza turejee vitabu gani. Zaidi nikupongeze kwa kazi njema
Post a Comment