Saturday 10 May 2014

MALEZI BORA YA WATOTO Na Changamoto ya kizazi hiki





Imeandaliwa na
Mchungaji
 Lupakisyo Mwakobela Mwakasweswe



Barua Pepe:   lmwakasweswe@yahoo.co.uk
Simu ya mkononi: +255- 0764 150 391
Blogi:  Mwakasweswe.blogspot.com

Utangulizi


Katika fundisho hili tutajifunza malezi bora ya watoto katika nyumba za watu wanamwamini Mungu. Ni wakati ambapo wazazi wengi wamekata tama ya mazi ya watoto wao. Kumekuwa na changamoto nyingi kwa jinsi yakuwa lea watoto wanaoishi katika kizazi chetu. Imekuwa kwamba watoto nao wamejifunza na kuiga tabia ambazo wazazi wanashangaa kwamba wametoa wapi? Limekuwa gumzo kanisani kwenye anyumba ya ibada , barabarani , katika taasisi mbalimbali mjadala ukiwa ni jinsi gani watoto wasikuhizi walivyo na tabia za ajabu .
 Kwa kuzingatia umuhimu wa ujenzi wa tabia  mwandishi na mjumbe wa Mungu anaandika katika kitabu cha Elimu ya kikiristo uk 165 anasema “ Ujenzi wa tabia ni kazi ya muhimu kuliko zote alizopewa mwanadamu; na kamwe kabla umuhimu wa kujifunza kanuni kwa makini haujakuwapo kama ulivyo sasa.”
 Katika somo hili tutajifunza mpango wa Mungu kwa uzazi wa watoto, pia  tutajifunza na kuona wapi tumefanya makosa kama wazazi katika ujenzi wa tabia za  watoto wetu.
Malezi ya watoto hayakosi changamoto ambazo wazazi wanakutana nazo, yaweza kuwa kupitia maisha na tabia walizojifunza kutoka kwa marafiki yaani makundi au kwa kuzipata kupitia malezi ya wazazi wao. Changamot hizi ni pamoja na watoto kujiingiza katika unywaji wa pombe, kuacha maisha ya ibada, kuvuta sigara na bangi, kuwa na mahusiano ya kingono kati ya jinsia mbili na jinsia moja yaani ushoga, kutopenda masomo, kuwa na ujauzito usio halali, magonjwa ya zinaa na Ukimwi.
Somo hili halitajadili maendeleo ya mtoto katika ukuaji wake bali  litazungumzia malezi bora ya ujumla kwa watoto. Ni tumaini langu kwamba baada ya somo hili, kila Mzazi atajua wajibu wake kwa malezi bora ya watoto wake, kila mzazi atahisi mahali alipo fanya vibaya katika malezi ya watoto wake pia atafanya yampasayo kutenda  ili kuwa na  malezi bora ya watoto wake.

Mpango wa Mungu kwa wazazi;  Adamu na Hawa


Mwanzo 1:27,28  Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. 28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi. Mpango wa Mungu  ulikuwa kumuumba mwanadamu kwa mfano wake, na kwa maana hiyo mwanamke na mwanaume  ni mfanao wa Mungu.

Unaweza kujiuliza kwamba Mungu anafanana na mwanamke au mwanaume, hilo si swala la kujadili kwani Mngu anaumba mtu kwa namna yake ya asili. Mwanadamu ameumbwa akiwa mkamilifu katika njia zake mpaka pale dhambi ilipo ingia na kumfanya mwanadamu apoteze sura ya ukamilifu wa Mungu.

            Mungu alifahamu kwamba hawa wazazi wangekuwa mfano bora katika maisha yao mbele ya watoto wao, watoto wasingehangaika kuyafamu yaliyo mapenzi ya Mungu. Tunayo furaha kwamba baada ya anguko la mwanadamu Mungu alifanya mpango wa ukombozi, Yesu kristo akaja akafa badala ya mwanadamu, mwanadamu akahesabiwa kwamba ana haki kwanjia ya Yesu kristo. Yohana 3:16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.Wazazi wanaqodumu kuwa waaminifu wameahidiwa kuto potea bali wamehakikishiwa uzima wa milele.

Katika kitabu cha mwanzo 1:27, 28 Mungu akawabarikia wazazi wetu wa kwanza, Mungu akawapa wajibu wazazi wetu wa kwanza , wazazi hawa alipewa kila kitu kilcho kuwa muhimu kwa maisha yao. Mungu anajuwa kilicho muhimu katika maisha yetu pia, aliweza kuwapatia wazazi hawa vitu maalumu vya kula hata vya kutunza tu, kisha baada ya kuwabarikia, biblia inasema Mungu akawaambia, Zaeni .
Kuzaa ni agizo la Mungu tangu katika bustani ya edeni, kuzaa ni agizo baada ya kubarikiwa, unaweza kugundua kwamba Mungu hakutoa agizo la kuzaa mpaka kwanza alipo wabariki wazazi wetu, Mungu aliwapa vitu muhimu vizuri vya kuwa navyo kabla ya kuzaa. Mungu wetu ni Mungu wa utaratibu, hachanganyi mambo kama ambavyo mwanadamu anachanganya mambo, hebu angalia, mzazi anajikuta ni mjamzito bila kujua nini cha kumpatia motto anayetarajiwa kuzaliwa.
Siyo ajabu wazazi wengi wameanza maisha bila kuju kwamba Mungu amewabariki kwa kuwa na vitu vya kuanzia maisha hasa watoto wanapo anza kuja duniani, hebu fikiri mzazi, Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, zaeni. Je kabla ya kuzaa ulijiandaa kiasi gani kuhusu maisha ya motto au watoto wako? Mungu hatoi agizo la kuzaa kabla ya kukubariki.
Wazazi wengi wameiga kutoka kwa wazazi wengine na kusema kila motto huja na bahati yake, hili limesababisha watoto wengi wamezaliwa katika mazingira ya hatari sana, wengi hawajakutana na nepi kama wengine wengine wamektana na vipande vya kanga nk. Agizo la Mungu ni kubariki na kutoa agizo la kuzaa. Agizo la kubariki tumbo la uzazi liko palepale lakini hakuagiza uzazi usio na mpango. Mungu anapoagiza, Mkaongezeke , alimaanisha vizazi na vizazi na kuongezeka kwa namba ya wanafamilia yako nay a jirani yako, pia alimaanisha Kujaza nchi, Mungu anapendezwa na watu wanoweza kumwabudu kumsifu. Mungu alijua watu wengi watakuwepo ambao watatangaza habari zake katika ulimwengu huu. Mimi na wewe mzazi ni matokeo ya ongezeko la watu duniani.
Kwa taarifa ya sensa ya mwaka  2012 Watanzania tumefikia idadi ya watu 42,000,000( milioni arubaini na mbili) ongezeko hilo ni changamoto kwa serikali na kwa familia, kwani linatakiwa ongeko la miundo mbinu, chakula, maji, barabara , makazi mazuri , mpango mzuri wa uzazi, Magonjwa ya wakina mama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano nk.
Agizo la  Mungu kwa wazazi wetu wa kwanza  ,waliambiwa waweze kuitiisha nchi  Mwanzo 1:28  na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi. Wajibu huu mkubwa wa kutiisha ni wajibu wa kila mzazi, kuhakikisha kwamba vinatii maagizo yako, kutawala na kuhakikisha kila kiumbe kiendacho juu ya nchi kinatawaliwa nawe, si ajabu ukashangaa kwamba viumbe wengine ambao bado hawajazaliwa utakuwa na wajibu wa kuhakisha maisha yao yanatunzwa vizuri na wewe, zaidi sana wewe kama mzazi ndiye unaweza kutiisha hata ujauzito ukatungwa kipindi utakacho panga, kumbe kama mzazi utakuwa tayari kuendelea kumpatia elimu ya Mungu mtoto wako uliye mzaa.
Bahati mbaya wazazi wengi tumewaleta watoto duniani bila utaratibu na kujenga hoja kwamba bado nina nguvu za uzazi na mayai bado yapo, hilo ni sahihi kabisa lakini tukasahau kwamba Mungu wetu ni wa utaratibu, anabariki kwanza na anatoa agizo kwamba Zaeni. Unaweza kupita mitaani na usishangazwe na majina ya watoto kama vile Sikujua, Mapenzi , Yote haya ni kujipa matumaini kwamba Mungu alipanga mtoto huyu azaliwe pasipo kujua, na wakati mwingine tumeseam ni mapenzi ya Mungu, yote hayo ni sawa lakini tiukumbuke kwamba Mungu ni Mungu wa utaratibu.
Ninajaribiwa kuamini kwamba ilipo fika wakati wa kugawa mali kwa wtoto, wazazi wetu wa kwanza hawakupata tabu kwa sababu kila kilicho kuwa hitaji la mtoto lilifanyika. Mwanzo 4:2 Akaongeza akamzaa ndugu yake, Habili. Habili alikuwa mchunga kondoo, na Kaini alikuwa mkulima ardhi. Hebu chunguza hapa kwa makini, Baada ya wazazi wetu kuongeza motto , Habili alikuwa mtaalamu wa mifugo na Kaini alikuwa mtaalamu wa Shamba. Wazazi hawa walipoombwa mali Ninaamini walitoa kwa moyo wote, Habili walimpatia kondoo za kumtosha , na kaini walimpatia eneo kumbwa la ardhi.

Watoto ulionao na unaopanga kuwaleta duniani  wanacho kitu cha  kuwatosha kutoka kwako? Umebarikiwa kiasi gani kuweza kuwaridhisha watoto wako. Unauelewa kiasi gani wa neno la Mungu kama mafundisho awali kwa watoto wako, umejiandaa kiasi gani kwa malipo ya ada ya shule na vyuo, unamaandalizi kiasi gani ya Vyakula katika nyumba yako.

 Mungu wetu anautaratibu mzuri. Tambua mbaraka wako kabla ya kuzaa. Mwandishi E.white akieleza habari hii anasema   “Wako wazazi  ambao, bila kufikiri kama waweza kuwatendea ipasavyo jamaa kubwa ama sivyo, huzijaza nyumba zao watoto hawa wadogo wasioweza kujisaidia wenyewe, wenye kuwategemea tu wazazi wao kwa matunzo na kwa mafundisho. Hili ni kosa kubwa baya, si kwa mama tu, bali kwa watoto wake na kwa jamii ya watu mtaani. Mtoto mikononi mwa mama mwaka kwa mwaka ni udhalimu mkuu kwake. Hupunguza , na mara nyingi huharibu starehe na kuongeza uchovu wa kazi nyumbani. Huwanyang’anya watoto matunzo, elimu na furaha amoto ulimwenguni ambayo wazazi wangeiona kuwa ni wajibu wao kuwapa  (Wazazi) wangefikiri kwa makini riziki wawezazo kuwapatia watoto wao. Hawana haki kuzaa watoto ulimwenguni kuwa mzigo kwa wengine”.  AH 159 - 164

Wazazi wengi wamejikuta wakiwatukana watoto wanapohitaji mambo muhimu ya shule. Nilishuhudia mzazi mmoja akiombwa na motto wake penseli ya kuandikia shuleni naye akamjibu kwamba “wewe unadhani si tunakunya hiyo penseli”. Niliamua kunyamaza ila niliumia sana, je motto amliumia kiasi gani? Unadhani mapenzi ya mtoto huyo kwa mzazi wake huyo yakoje sasa.

Wazazi wengi wamepandikiza tabia mbaya kwa wtoto wao kwa jinsi walivyo walea katika maisha yao ya utoto. Watoto wengi walijibiwa vibaya na kupigwa kwa sababu ya wazazi kukosa vitu au mali kwaajili ya kusaidia elimu ya watoto wao. Mungu anampango mzuri kwako wewe unayaendelea kuzaaa au unaye anza kuzaa, Panga uzazi wako maana Mungu anabariki kwanza ndipo anaagiza mwanadamu azae

 Malezi bora yanaendana na mpango mzima wa maandalizi ya ujauzito na kuendelea kulea katika njia njema. Tabia njema zitafundishwa kwa watoto endapo mzazi utafahamu maendeleo ya tabia za watoto kutokana na mazingira ya kurithi na katika mazingira.

Malezi na Tabia za watoto kwa kurithi


Kumekuwa na changamoto kubwa sana kwa wazazi katika kurekebisha tabia za watoto wao ambazo ni matokeo ya kurithi. Watoto wengi wamezaliwa na tabia za wazazi wao au babu zao , kwa mfano hali za moyo, akili, tabia za maumbile ya nje  kwa mfano rangi za macho na ngozi, mfumo wa meno, urefu, uzito, pamoja na mihemuko.
 Mara zingine motto anaweza kuwa hajiwezi darasani ,hii inaweza kuwa sehemu ya kurithi, hii yaweza kusababishwa na mambo mengi ambayo yanahusiana tangu utungaji wa mimba na malezi baada ya hapo. Maandishi ya liyovuviwa  yanasema “ Ikiwa kabla ya kuzaliwa mtoto wake, mama mwenyewe ni mfisadi, kama ni mchoyo, mwenye harara na mkali, tabia hizi zitaonekana kwa mototo . Hivyo watoto wengi wamerithi maelekeo mabaya wasiyoweza kuyashinda ila kwa shida sana “AH 255 -267                                                                                                
Kwa namna nyingine , mzazi asingeharakisha kutoa adhabu kwa motto wake kabla ya kukaa na motto wake na kumweleza makosa yake. Mara zote isinge kuwa bora kuadhibu bila kujua kwamba ulifundisha jambo unalolichukia kwa motto wako, endapo amejifunza kutoka nje yako, pia ni vyema ukajiridhisha na kujua jinsi ya kuongea naye. Maandishi ya uvuvio yanasema “ Akili za watoto ni nyepesi, nao hutofautisha sauti za uvumilivu, na upendo na amri kali ya hasira, ambayo hukausha upendo na nia njema mioyoni mwa watoto. Mama Mkristo wa kweli hatawafukuza watoto wake machoni pake kwa ukali wake na kukosa huruma. “AH 232 -254

Malezi Na Tabia za watoto kutokana Na Mazingira

Sababu za Maombi katika Familia

            Kama kuna jambo la muhimu katika familiani suala la ujenzi wa tabia watoto kwa kupitia Nen la Mungu. Mithali 22:6 Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mze.   Kumbukumbu la Torati 6:7 nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.Kumbukumbu la Torati 11:19 Nayo wafunzeni vijana vyenu kwa kuyazungumza uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.
Wazazwote wangefuata mashauri haya , watoto wengi wangaliweza kuwa na maisha bora, lakini hujachelewa ” Baba na mama, kila siku asubuhi na jioni wakusanyeni watoto wenu karibu  nanyi, kwa maombi ya unyenyekevu, inueni mioyo yenu kwa Mungu mpate msaada.” 7T 32-44

Sababu za kiuchumi

            Wazazi wengi wamekuwa wakijishughulisha na maswala ya kiuchumi ili kukidhi mahitaji ya watoto wao. Imekuwa kwamba wazazi wengi wameshughulika lakini matokeo yake yamekuwa hafifu hata kushindwa kutosheleza mahitaji ya watoto wao. Hii yawezekana kwa kukusa kujituma (uvivu) kutokuwa na maarifa ya kubuni njia za kupata fedha za kutunza familia zao.


Taifa la Tanzanai akwa ujumla limekuwa likisisitiza kuhusu elimu ya ujasilia mali ambayao inamfanya mtu kuwa mbunifu na kuanza kufanya kitu , kwa uchache sana wengi wamepuuza elimu hii na wamebaki wakiwa na sababu za kutokuwa na mali za kulea watoto wao, hii ni makosa kwa mzazi.
            Sababu za kiuchumi zinahusisha ni kwa jinsi gani mzazi umefanikiwa kuwa na kipato chako binafsi, kuwa na uwekezaji, utunzaji wa fedha kwa ajili ya matumizi ya baadaye,kuwa na madeni ambayo yamesumbua familia nyingi hata kukosa mahitaji muhimu, kukosa katika hili kumewafanya wazazi wengi kukusa vitu muhimu yaani chakula bora, afya nzuri ambavyo ni muhimu sana kwa ukuaji wa mototo.
            Maandishi ya uvuvio yanaeleza kwamba “Watu wengi walio maskini ni maskini kwa sababu hutumia fedha zao mara tu wazipatapo” AH 392
 Akiendelea anasema “Wale wanajidai Kwa hali yoyote kuwa wenye utauwa, yawapasa kujivika mafundisho wanayo yakiri, wala wasitoe nafasi kwa neon la Mungu hutukanwa kwa sababu ya mwenendo wao wa kutojali. Mtume anasema, “ Msiwiwe na mtu cho chote” 5T179 – 182

Sababu za mlo

Sababu za kukosa chakula chenye viini lishe, wazazi wengi wamejikuta watoto wao wakiwa na tabia tofauti katika makuzi yao. Kukosa mlo kamili ni kosa kubwa katika malezi ya watoto. Hata Tanzania , tumebarikiwa kuwa na chakula cha mboga  matunda ,nafaka, vyakula ambayo  kama vingetumiwa vizuri vingeweza kusaidia katika makuzi ya watoto na ujenzi wa tabia njema. Magonjwa mengi kama vile kuishiwa damu , utapiamlo , na magonjwa mengine vimechangia sana katika maendeleo mabaya  ya ukuaji wa akili za watoto.
 Tabia za watoto wengi zimeharibiwa na jinsi walivyp lelewa na kwa jinsi walivyo achwa hivyo , leo tunaweza kushuhudia watoto wengi hata watu wazima wakifanya mambo tofauti kwa sababu tu ubongo wao haukuandaliwa vizuri katik aumri wao mdogo.

Sababu za Magonjwa na  kuugua

            Watoto wengi wameathirika akili zao Kwa kuwa na magonjwa ambayo yameathiri akili zao, mihemuko yao na makuzi ya kijamii. Magonjwa Kama ya mifupa, baridi yabisi, kuwa na usumbufu wa kutosikia vizuri. Yote haya yanasababisha tabia za watoto ziwe tofauti na makusudio ya mzazi.
 Inapasa wazazi kuwa makini katika kujikinga na magonjwa mbalimbali yanayoweza kunyemelea watoto wako. Wazazi wengi wamepuuzia kuwapeleka watoto wao katika hosipitali, kumekuwa na matangazo mengi ya kupeleka watoto kwenye chanjo lakini ni wachache wanao itikia mwito huu. Hebu kila mzazi atambue wajibu wake.

Sababu za Mazoezi ya Viungo

            Mazoezi ya viungo ni dawa nzuri Kwa afya yakila mtu. Watoto wanafaidika Sana kwani mazoezi yanasaidia kupunguza msongo wa maisha, yanasidia katika kujiamini, kuosa mazoezi kumefanya watoto wengi kudumaa, wamejikuta afya zao zikiwa mbaya, wameshindwa kukuwa kwa ulinganifu uliobora.

Sababu za Mila na Desturi za jamii.

            Katika eneo hili, tamaduni zimechangia kutengeneza tabia za watoto, kwa mfano jamii nyingi zimekuwa na ubaguzi wa jinsia.
 Kwamba watoto wakiume wamechukua sehemu ya juu sana na kuonekana wanafaida kubwa katika jamii kuliko wana wa kike. Watoto wengi wa kiume wamekuwa wakishindwa kufanya kazi ndogo za nyumbani kwa kutegemea kuwapo kwa wasichana. Watoto w kike wameshindwa kupata elimu kwasababu wazazi wengi wanadhani watoto wa kike ni wa kuolewa tu. Maandiko matakatifu katika kitabu cha Mathayo 25:40 Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi. Swali kubwa Kwa wazazi leo, tunawafundishaje watoto wetu katika mila na desturi zetu? Tabia zao zinaathirika kwa kiasi gani? Yesu anasema kwa kutenda kwetu.
 Hii imefanya tabia za baadhi ya watoto wa kike kutojiamini katika maisha yao na kujiona kwamba wao ni wa kuolewa tu hivyo huanza tabia za kutafuta kuolewa hata kabla ya umri unafaa. Wazazi wangejifunza kwamba Mungu hana Upendeleo wala ubaguzi. Kwa kufanya hivi ni kumkosea Mungu.
Tamaduni hizi zimekumba nyumba za ibada. Wazazi walio wafundisha watoto wao kwamba wao hawafai kusimama mbele za wana wa kiume mpaka sasa wamekuwa na tabia ya woga, wa meshindwa kushiriki kikamilifu katika kazi za kanisa na shughuli mbalimbali za mahali pa ibada ya Mungu. Tabia hizi ni matokeo mabaya ya kuwa na tamaduni ambazo hazina ukubali wa maandiko matakatifu ya Mungu kwani Mungu alipoumba mwanadamu alitaka kila mtu amwabudu yeye.  
Maandiko matakatifu katika kitabu cha Ufunuo wa Yohana 14:7 akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji
Hakuna aliyeachwa katika kusujudu mbele za Mungu, hakuna aliyeachwa katika kumcha Mungu na kumtukuza kwa sababau hukumu italetwa kwa kila mtu, haijalishi ni jinsia ya kike au ya kiume, hivyo basi tamaduni mila na desturi zisifanye wazazi wengi kuwafundisha watoto tabia zitakazo haribu maisha na wokovu wao.

Changamoto za malezi ya watoto katika kizazi hiki

 Unywaji wa pombe ,Katika ulimwengu huu wa sayansi na technolgia, kuacha maisha ya ibada, Uvutaji wa sigara, bangi,( madawa ya kulevya) kuwa na mahusiano ya kingono kati ya jinsia mbili na jinsia moja yaani ushoga, kuwa mtoro wamasomo, kuwa na ujauzito usio halali na kupata Magonjwa ya zinaa na Ukimwi.
Pamoja na changamoto hizi, mzazi anapaswa kumwombea motto wake ili kwamba Mungu aepushe balaa hizi. Wakati Fulani unaweza ukapatwa na majaribu kwamba mtot wako amejiingiza katika moja wapo ya hayo, kumbuka endapo ulimkabidhi mikononi mwa Mungu, Mungu bado anazungumza pamoja naye maana hata acha mafundisho aliyopewa na mzazi hata atakapo kuwa mzee. Endelea kuomba na akuomba na kuomba.

0 comments:

Post a Comment