Saturday 10 May 2014

UVIVU NA MADHARA YAKE


Pr.  Lupakisyo Mwakobela Mwakasweswe

Kutoka 20: 8, 9 ,10 Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. 9 Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; 10 lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.

Utangulizi
Mungu alipo umba dunia aliiweka siku ya sabato iwe ishara ya uumbaji. Mungu aliamuru siku ya sabato iwe pumziko baada ya kazi za wiki, Mungu alijua kwamba mwanadamu aliihitaji kufanya kazi ili ale. Si ajabu ukamkuta kijana ambaye anazunguka zunguka bila kufanya kazi, hii ni kukosa kuamini kile Mungu aliocho sema Siku sita fanya kazi. Kukosa kufany kazi ni kosa kubwa kwa sababu Uvivi huleta balaa kubwa katika maisha ya mtu, serikali , kanisa na jamii kwa ujumla. Mungu atusaidie kupiga vita uvivu maana ni chanzo cha dhambi.

Uvivu Na Madhara yake
            
Mjumbe wa Mungu akiandika alisema “ Nimeonyeshwa  kuwa dhambi nyingi zimetokana na uvivu. Mikono na bongo hodari kwa kazi hazina nafasi kusikiliza kila jaribu ambalo adui huwaletea, lakini mikono na bongo zenye uvivu ziko tayari kabisa kutawaliwa na shetani. Akili isiposhughulishwa vizuri, hufikiri mambo mabaya yasiyo faa.” 1T 395
            Kama kuna jambo la hatari kwa maisha ya mwanadamu hasa vijana, ni kuwa mvivu, Uvivu ni hali ya kutopenda kufanyakazi au kufanya kwa kiwango hafifu bila kujali. Mtu mvivu hapendi kushughulisha akili yake hivyo anajikuta akili yake inawaza vitu vyepesi na ambavyo vinatumia hisia zaidi.
            Hisia zinapopata nafasi hufanyiwa kazi, kwa mfanao mtu atajisikia kwenda kuiba maana kwake ndiyo njia rahisi kupata, mwingine atajisikia kuzini tu maana mwili wake hauna uzio wa tama yake, maana mawazo yake yame lemewa na hisia chafu, mwingine atajikuta anawaza kunywa pombe maana hana kitu cha kumchangamsha ,mwingine atajikuta yuko kwenye makundi ya hatari hata ya kuvuta sigara , bangi , madawa ya kulevya, na ujambazi wa aina mbalimbali.
Mungu aliahidi kila mtu afanye kazi iliafurahie maisha katika ulimwengu huu. Vijana wengi huwa wavivu hata katika masomo yao , hawajibidishi kusoma, wanaishia kunakili daftari za wenzao hivyo kuwadanganya wazazi wao kwamba wanasoma. Kipindi cha likizo watoto  na vijna wengi hutumia kucheza michezo tu , kuangalia Luninga n nakupenda safari zisizo na maana, mara kwa bibi, kwa mjomba kwa kaka, anachokwenda kufanya ni kulala tu. Imekuwa mtu mvivu hupenda kula tu neon la Mungu kupitia mtume paulo linasema, 2 Wathesalonike 3:10 Kwa kuwa hata wakati ule tulipokuwapo kwenu tuliwaagiza neno hili, kwamba ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula.

Maswali ya kujadili
1.      Uvivu ninini?
2.      Mimi ninamfahamu mtu mvivu?
3.      Kuna aina ngapi za uvivu?
4.      Je nini madhara ya kuwa mvivu nyumbani
5.      Ninini madhara ya kuwa mvivu shuleni
6.      Ninini madhara ya kuwa mvivu na nimefikia muda wa kuoa au kuolewa?
7.      Mungu anasema nini katika swala la matoleo/sadaka nitapata wapi
8.      Nikiwa mvivu kazini nini kitanipata kutoka kwa bosi wangu?
9.      Nini kilicho madai ya Mungu katika utunzaji wa Sabato?
10.  Nisipofanya kazi siku sita nitapata madhara gani?
11.  Nifanye kazi gani mimi mwanafunzi wa shule ya msingi wakati wa likizo?
12.  Mimi mwanafunzi wa sekondari nifanye kazi gani za kipato wakati wa likizo au wakati mwingine?
13.  Nisipofanya kazi nini kitanipata?

Msaada wa Mafungu kwa mvivu

Mithali 19:15 Uvivu humtia mtu katika usingizi mzito; Na nafsi yake mvivu itaona njaa.

Mithali 31:27 Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; Wala hali chakula cha uvivu.

Mhubiri 10:18 Kwa sababu ya uvivu paa hunepa; Na kwa utepetevu wa mikono nyumba huvuja
Mithali 6:6 Ewe mvivu, mwendee chungu, Zitafakari njia zake ukapate hekima.

Mithali 6:9 Ewe mvivu, utalala hata lini? Utaondoka lini katika usingizi wako?

Mithali 10:26 Kama siki menoni, na kama moshi machoni, Ndivyo alivyo mtu mvivu kwao wamtumao.

Mithali 12:24 Mkono wa mwenye bidii utatawala; Bali mvivu atalipishwa kodi.

Mithali 12:27 Mtu mvivu hapiki mawindo yake; Bali mwenye bidii anazo mali za thamani.

Mithali 13:4 Nafsi ya mtu mvivu hutamani asipate kitu; Bali nafsi ya mwenye bidii itanenepeshwa.

Mithali 15:19 Njia ya mtu mvivu ni kama boma la miiba; Bali mapito yao wenye unyofu hufanyika njia kuu.

Mithali 18:9 Yeye naye aliye mvivu katika kazi yake, Ni ndugu yake aliye mharabu.

Mithali 19:15 Uvivu humtia mtu katika usingizi mzito; Na nafsi yake mvivu itaona njaa.

Mithali 19:24 Mtu mvivu hutia mkono wake sahanini; Ila hataki hata kuupeleka kinywani pake.

Mithali 20:4 Mtu mvivu hataki kulima wakati wa baridi; Hivyo wakati wa mavuno ataomba, hana kitu.

Mithali 21:25 Matakwa yake mtu mvivu humfisha, Kwa maana mikono yake hukataa kufanya kazi.

Mithali 22:13 Mtu mvivu husema, Simba yuko nje; Nitauawa katika njia kuu.

Mithali 24:30 Nalipita karibu na shamba la mvivu, Na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili.

Mithali 26:13 Mtu mvivu husema, Simba yuko njiani, Simba yuko katika njia kuu.

Mithali 26:14 Kama vile mlango ugeukavyo katika bawaba zake; Kadhalika mtu mvivu katika kitanda chake.

Mithali 26:15 Mtu mvivu hutia mkono wake sahanini; Kwamchosha kuupeleka tena kinywani pake.
Mithali 26:16 Mtu mvivu ni mwenye hekima machoni pake, Kuliko watu saba wawezao kutoa sababu.


Mungu akubariki unapoamua kuachana na uvivu.

0 comments:

Post a Comment