Thursday 15 May 2014

UTAMJUAJE MTU MWENYE KUTAKA MAFANIKIO KATIKA BIASHARA/MRADI WAKE?


BIASHARA/MIRADI


Mwezeshaji: Pr Lupakisyo M.Mwakasweswe



JE UNAMFAHAMU WALT DISNEY?

Walt Disney: Walt alifukuzwa kutoka jiji la Kansas ambako alikuwa anashughulika na uandishi wa habari  ambako alionekana kuwa ni mtu asiyefanya mambo kwa haraka, alionekana mlegevu asiye mbunifu  kama mtoto mdogo . Kwa sasa ni mtu maarufu,  mtengenezaji wa picha zinazotembea (motion picture ) katika ulimwengu wote amepokea tuzo  kuu sana zinazo mpatia heshima kubwa sana duniani.

UTAMJUAJE MTU MWENYE KUTAKA MAFANIKIO KATIKA BIASHARA/MRADI WAKE?

Majibu ya swali  kama yalivyo jibiwa na washiriki wa semina ya Uwakili na Ujasiliamali
katika Kanisa la Wa adventista wa Sabato Ngongongare  - Arusha Tarehe 1/4/2014

1.      Anaweka malengo katika biashara yake na namna ya kuyafikia malengo.
2.      Anajuhudi katika biashara yake hapotezi muda anawajibika kikamikifu.
3.      Anaongeza juhudi na kutumia fedha yake vizuri kwanza Mungu.
4.      Anapokea ushauri kutoka kwa watu wengine wenye mafanikio.
5.      Anatumia kauli nzuri ya kuvutia wateja wake. (Ana uso wenye tabasamu).
6.      Anatumia akili ya kujua ni wapi ataweza kufanikiwa tena.
7.      Anakuwa mtu wa maombi biashara yake.
8.      Anakuwa mdadisi kwa wengine
9.      Anaamka Asubuhi na mapema kazini.
10.  Anamshukuru Mungu kwa kidogo apatacho na kukiendeleza hakatishwi tamaa.
11.  Ni mtu mwenye kuthubutu kufanya mambo.
12.  Mjasiri na mwenye kujiamini kwakile anachofanya.
13.  Mvumilivu
14.   Mbunifu.
15.  Ni mtu anaekubali kushauriwa
16.  Mkweli
17.  Akipata wazo hulifanyia kazi mara moja.
18.  Hukubali ushauri kwa watu waliofanikiwa.
19.  Hubadilika kulingana na hali ya uchumi.
20.  Baada ya mafanikio hubuni biashara nyingine ili kuongeza kipato.
21.  Huwa nakini katika mahesabu ya kazi ili kujua faida na hasara.
22.  Atajali anachokifanya.
23.  Atambue faida na hasara katika mazingira yaliyomzunguka.
24.  Atahitaji Elimu ya ziada ili kufanikisha kazi yake. 
25.  Atakua  na ratiba ya kazi  yake atatunza .
26.  Atakua mbunifu kutokana na mazingira.
27.  Atalinda mtaji.
28.  Atajali masharti ya biashara.
29.  Awe anafahamu mahitaji ya jamii iliyomzunguka.
30.  Awe tayari kujifunza/ kutafiti toka kwa wenzake.
31.  Awe na uaminifu katika shughuli zake baina yake na Mungu pamoja wateja wake.
32.  Asiwe na muda mwafaka katika kuanza biashara yake na wala muda huo usiwe wa kubadilikabadilika.
33.  Awe na bidhaa inayokubalika katika jamii yake.
34.  Awe mwaminifu katika kulipa kodi (TRA).
35.  Awe msafi binafsi na mazingira yake yaliyomzunguka.
36.  Awe na Elimu juu ya shughuli anayotaka kuanza.
37.  a) Usiogope kuanza (kuwekeza 
38.   Udadisi/ kutafuta elimu.
39.  Ana fikra chanya.
40.   kujijali / na kujali watu
41.  Mtendaji sio maneno
42.   Mwaminifu asiwe mdanganyifu.

NYONGEZA YA MWEZESHAJI
1.      Hawapendi hasara kubwa
2.      Hupenda kubeba majukumu huona kwamba kila anachpata ni matkeo ya juhudi zake
3.      Hupenda kujua matoke ya nguvu zake
4.      Ni wabunifu wa kupanga mbinu mbalimbali za shughuli zao.
5.      Ni wavumilivu kwa matatizo yanayotokea
6.      Ni mtu wa vitendo kwa mambo wanayoyapanga
7.      Si watu wa kuridhika kwa kila ambacho wanapanga

 MFANYA BIASHARA AU MTU MWENYE MRADI ANAYEFANIKIWA;
1.      Anaanza biashara yeyemwenyewe – haajiri mtu kwanza
2.      Hupenda watu maana ndiyo wateja wake
3.      Ni watu wanaojua kuongoza
4.      Hupenda kuna shughuli aliyo ianzisha imekwisha
5.      Hufanya kazi kwa malengo
6.      Huwa na mipango
7.      Wanamaamuzi ya haraka lakini ya busara
8.      Hupenda kijitegemea
9.      Huwa hawajui iwapo biashara zao zitafanikiwa wanapenda kuwajibika
10.  Wana mawasiliano mazuri na wenzao/wateja
11.  Hupenda kubadilika na wanajiamini.


Traumatized Children in the Family





 Traumatized Children in the Family

Pr. Lupakisyo M .Mwakasweswe

 BATH. PGDE. MSC Psychology


 Introduction
 According to Andrews (2010), when a child experiences a traumatic upbringing where they are deprived of predictability, trust, nurturing, love and hope, childhood becomes toxic, unpredictable and abusive. Their world may be witness to violence, crime, drugs and a parental style that is full of ridicule, fear and insults. Following a trauma experience, an individual may begin to perceive the world as an unsafe place, living in a state of constant arousal. This can result in changes in the brain, which are triggered by stress functions and may alter the way we view others and ourselves. As our perceptions shape our behaviors, if the world or those around us are perceived as unsafe, this may result in an increase in anxiety or aggression, altering or impairing contact with others (Steele & Raider, 2009). According to Perry (2001), the most significant relationship in a child’s life is the attachment to their primary caregiver, acting as an emotional template for future relationships. When it is conflict-ridden, with rejection typically at the core, the outcome may lead to fragile foundations for future relationships. Mate (2008), suggests that individuals with addictions are constantly seeking something outside of themselves to alleviate their insatiable need for relief and need for relief and fulfillment. It is as a result of this longing and emptiness that individuals pursue substances or other self-harming or self-soothing behaviors, with the hope that it will provide some relief. Andrews (2010), further supports this notion in stating that children who have been neglected early in life will experience future life from the understanding of the need to fight for survival at every level, physically, emotionally, spiritually and psychologically. It is out of this fight for survival the litany of behaviors begins, behaviors that will temporarily give relief from fear and the pain that they suffer.

 Reference 

 Andrews, E. (2010). Being trauma informed [power point slides]. St. Catharine, Ontario, Canada.

 Mate, G. (2008). In the realm of the hungry ghost: Close encounters with addiction. Toronto, Ontario, Canada: Random House.

 Perry, B. D., & Szalavitz, M. (2008). The boy who was raised as a dog: and other stories from a child psychiatrist’s notebook. New York, NY:

 Basic Books. Schore, A. N., (2001). Effects of a secure attachment relationship on right brain development, affect regulation, and infant mental health. Infant Mental Health Journal, Volume22 (1- 2), 7-66. S& Raider,

Sunday 11 May 2014

MUZIKI NA UIMBAJI KATIKA IBADA




UTANGULIZI


Muasisi Mkuu wa Muziki na Uimbaji ni Mungu.  Muziki uliumbwa kwa matumizi matakatifu, kuinua mawazo kwa mambo yaliyo safi, mema na kuamusha katika moyo ibada na Shukurani kwa Mungu.”   Ellen White anaendelea kusema: “Muziki ni moja ya sanaa ya pekee.  Muziki mzuri hauleti tu burudiko la rohoni, bali pia bali huyainua akili katika vimo vya juu kwa mambo mazuri.  Mungu mara nyingi ametumia nyimbo za kiroho kugusa mioyo ya wadhambi na kuwaongoza kutubu. Kwa upande mwingine nyimbo zaweza kubomoa tabia adilifu na kututenga mbali na mahusiano   yetu na Mungu.”
Mama Ellen katika toleo hilo lililotajwa hapo juu ana haya ya ziada kuhusiana na kitengo ch a Muziki¨ Ellen G. White, Tumaini la Vizazi Vyote. Washington DC:  Review and Herald Publication Association p 73   Ibid.,  Uinjilisti wa Vitabu uk 43 Muziki waweza kuwa na mvuto mkumbwa kwa ajili ya mambo ya kupendeza, hata hivyo Hatujatumia huduma hii katika ibada kama ipasavyo. Mara nyingi nyimbo zimeimbwa   Kiholela bila mpangilio maalumu kufuatia matukio Fulani na mara nyingi wale wafanyao. Huduma hii wameachwa kufanya wapendavyo, na hivyo muziki hupoteza makusudi yake Kwa wale wanaosikiliza.  Muziki ni muhimu kuwa na Uzuri, mvuto na nguvu. Hebu sauti   Ziinuliwe kwa nyimbo za sifa na ibada. Utumiaji wa vyombo waweza kushirikishwa ili Utamu wake umfikie Muumbaji kama sadaka inayokubalika.” Ibid., uk 114
Muziki ulibuniwa na Mungui kwa ajili ya Ibada, Ukaagizwa na Mungu na , Ukabarikiwa na Mungu.  Wakati wa uumbaji nyota za asubuhi ziliimba na kwaya ya malaika wakapaza sauti zao kwa furaha.  (Ayubu 34:4-7).  Sehemu inayofuata tutaona jinsi Muziki ulivyovurugwa na adui.

HISTORIA YA ANGUKO AU UCHEPUKAJI WA VIWANGO VYA MUZIKI

VITA KUU BAINA YA KRISTO NA SHETANI

 KATIKA MUKTADHA WA MUZIKI


Vita kuu baina ya Kristo na Shetani ambayo ilianzia kule mbinguni ikafanya Lucifer MalaikaAliyekuwa kiongozi Mkuu wa Kwaya ya Malaika kule mbinguni alipotamani nafasi ya Mungu kama alivyotamka “nitakipandisha kiti changu juu kupita nyota za Mungu….nitafanana kama Mungu” Lucifa alitaka aabudiye. ( Isaya 14: 13,14 ) Mungu anataka aabudiwe na ndiyo stahili Yake kwa maana yeye ndiye muumbaji wa wote.  Shetani naye anataka aabudiwe
Na amefaulu Sana kupokea ibada ambayo haimstahili kwa kupitia kuwakilisha tabia ya Mungu vibaya kwa njia ya Muziki ambao ameuandika ili kusudi kulishinda kanisa la Mungu. Mdanganyifu mkuu akitambua ya kuwa muda wake ni mfupi sana amebuni njia hii ya kuwanasa Waadiventista Wanaodai kuwa wanamtii pamoja na kushika Sabato yake takatifu na kutunza amri kumi za Mungu kwa kupitia Muziki wa duniani ambao haumpi Mungu utukufu na Sifa badala yake humpa Ibilisi utukufu na Sifa japo unaimbiwa mbele ya kusanyiko takatifu la wasafiri wa mbinguni.
Ibilisi akitambua kuwa Ibada ndiyo njia rahisi ya kuliharibu kanisa la Mungu, amekusudia kuharibu utakatifu wa Muziki katika Ibada kuanzia katika bustani y Edeni. Vita kuu ya Muziki ambayo ilianzia katika bustani ya Edeni ni halisi, na hivyo ni muhimu kwetu kuelewa kama kanisa jinsi ambavyo uimbaji umeharibiwa leo na Yule adui, na sasa hebu na tufuatie historia ya Muziki na uchepukaji katika kanisa la Mungu la kweli.

ANGUKO LA KWANZA CHINI
YA MLIMA SINAI


Historia inaanzia na Waisrael wa Zamani (ambapo sisi tu Waisrael wa Kiroho).  Wakati walipokuwa wakisafiri baada ya Mungu kuwaokoa kutoka katika utumwa wa Misri  wakielekea katika nchi ya ahadi (Kaanani); wakati Musa alipoagizwa kukwea mlimani ili kupokea amri kumi za Mungu, watu (wakiongozwa na Kuhani Haruni) Walishangilia na kufanya ibada kwa ndama wa dhahabu, wakitoa sadaka, wakinywa na kucheza na kuimba. Muziki ambao uliambatana na Sherehe yao ulikuwa na Sauti kubwa na usio na mpangilio  kiasi ambacho Joshua alipokuwa akishuka toka mlimani pamoja na Musa wadhani ya kuwa illkuwa kelele za vita.
Lakini Musa Mtumishi wa Mungu akasema, La  hasha; ni kelele za watu wanaoimba. ( Kutoka 32:18). Jinsi watu walivyoimba na kucheza Haruni akawa akawaongoza  hata kubakia uchi wakimshangilia ndama wa dhahabu, ibada ambayo iliwaangusha katika zinaa. ( Kutoka 18:25 ).  Huu ulikuwa uasi wa Kwanza Mkuu kwa watu Wateule wa Mungu katika siku za awali kabisa za kanisa la Mungu. Muziki huu ambao ulibuniwa na Shetani ulikusudiwa kuwafanya watu kumvunjia Mungu heshima. Kama matokeo ya kumtii Yule adui na kukengeuka katika njia ya Mungu “wakaanguka watu wasiopungua elfu tatu.” (Kutoka 32:28)

ANGUKO LA PILI MASHARIKI MWA YORDANI


Takribani miaka kama arobaini (40) baada ya kuvuka bahari ya Shamu, wakati Musa Mtumishi wa Bwana alipokuwa tu amekwisha kutoa maagizo ya muhimu kabla ya kuvuka mto Yoridani ili kuingia katika nchi ya ahadi waliengesha mahema yao Baali- Peori upande wa mashariki  ufuoni mwa mto Yoridani Watu wa MUNGU kwa njia ya kujichanganya na mataifa wakaanguka katika anasa.
 Kwa mara NYINGINE TENA walishiriki katika Muziki wa mataifa na kucheza. Tendo hili likawapeleka mbali zaidi wakazama katika anasa, unywaji na ibada ya sanamu na muziki ule ukawafanya wakaanguka katika zinaa na kuanguka kiroho. Kwa njia hii Waisraeli walijiunga na ibada ya kipagani na kumuasi Mungu.  Na kwa mara nyingine tena adhabu kubwa iliwaangukia na zaidi ya watu elfu kumi waliangamizwa. Ibid. Wazee na Manabii 453-456

BAAL – PEORI YA KARNE YA LEO


Leo watu wa MUNGU kwa mara nyingine tena Waadiventista wa Sabato tupo tumepumzika katika mipaka ya Kaanani – Kaanani ya Mbinguni. Swali la Kujiuliza ni hili Je inawezekana kuona hali ile ya uasi kama ilivyokuwa katika Baal- Peori katika makanisa yetu ya sasa?  JIBU NI NDIO
Tupo katika kingo za Yordani tayari  kwa kuingia katika Kaanani ya Mbinguni ila tunachelewa hapo wakati tunangojea kumwagwa kwa Mvua ya Masika, na Kutoa kilio Kikuu cha kuutangaza ujio wa mwokozi wa haraka. Swali jingine la kujiuliza ni hili je wengi wetu makanisani hatujafanana na madhehebu mengine  hasa katika suala la ibada kwa njia y Muziki?  JIBU LA SWALI HILI PIA LAWEZA PIA KUWA NDIO.  Angalizo letu n ( 1 Yohana 2 :15)

ANGUKO NAMBA TATU ( 3 ) MARA TU BAADA YA MWAKA 1844


Baada ya tukio la Baal – Peori tunaposafiri kihistoria tunaingia wakati ambapo kanisa hili lilikuwa changa ndipo tu limeanza baada ya Mwaka 1844. Baada tu ya Mwaka 1844 wakati waumini watangulizi walipokuwa wanatazamia ujio wa Kristo kwa mara ya pili na kukosa kuja,
Kama vile inavyoweza fananishwa na Waisrael walipoanza safari yao ya kuingia katika kaanani ya duniani; watangulizi wenzetu walianza safari yao ya kuelekea katika kaanani ya mbinguni.  Katika kipindi hicho kulikuwa na hali Fulani ya utata katika historia ya Muziki wa Kiadiventista.  Ellen White anaeleza juu ya ekengeukaji uliojitokeza mnamo kipindi hicho kule Marekani. Katika sehemu nyingi Muziki wetu uliingiwa na hali ya makelele, kuruka na kucheza.  Mjumbe wa Mungu alitumwa na kusema yafuatayo: “ Nilitoa ushuhuda wangu kama onyo katika jina la Bwana nikikemea hali hii iliyojitokeza.”    Jambo la kutisha ni kuwa katika tukio hili baada tu ya mwaka 1844, watu walikaa uchi na matokeo yake yakawa kukengeuka na uovu ndio yalikuwa matokeo yake.
 Ki historia ni muhimu kuelewa ya kwamba kipindi hiki kanisa likiwa bado changa kuanzia mwaka ( 1865 – 1900 ) ndicho kipindi cha ugunduzi wa Muziki wa Jazz na Jazz ni jina linalosimama badala ya kujamiana (sexual intercourse ) ambalo lilichipuka katika nyumba za makahaba kule New Orleans, Lousiana .  Hiki ni kipindi ambacho marekani ilisumbuliwa na nyimbo hizi ambazo zilikuwa mpya na zikiwa na alama ukosefu wa adabu na kinyama pamoja na kuleta aibu.” Ibid., 2 Nyaraka Zilizochaguliwa (SM) uk 3  J. Simons.  Nyimbo za mporomoko wa Maadili, uk 35-39 
Angalizo hapa ni kuwa wakati kanisa la Mungu la kweli lilipokuwa limeanzishwa na bado changa, Mwana muziki aliyeanguka alikuwa pale tayari kuharibu utakatifu wa Muziki katika ibada ya kanisa ambalo analichukia sana.  Shetani anahitaji ibada yetu. Kwa kuanza kuandika Muziki mpotovu ambao pole pole ungelitoa kanisa katika njia yake sahihi na kuleteleza ujumbe wa malaika wa watatu.
Angalizo jingine ni kuwa Shetani ambaye ni Mwana Muziki Mkuu aliyeongoza kwaya  ya malaika watakatifu kule mbinguni, amegundua kile ambacho ana uwezo wa kukishambulia katika maisha ya mfuasi wa kristo nacho ni kutawala na ubongo wa binadamu kwani ni kwa njia hii ambayo Mungu anatumia kuwasiliana na binaadamu”
 Iwapo ubongo wa binaadamu ndio unaotawala maisha ya binaadamu hivyo basi kuna mantiki kwamba Shetani atafanya shambulizi lake la kwanza na la Mwisho kwa njia ya kutawala ubongo wa binadamu. Na iwapo Muziki ni zana ya muhimu sana katika matashi na tabia ya mwanadamu hivyo itakuwa kawaida kueleweka kuwa, Shetani atatumia Muziki kufikia malengo yake ya kumshambulia mfuasi wa kristo Ibid. uk 352

ANGUKO LA MSINGI WA MUZIKI SEHEMU YA NNE (4)
 KATIKA JIMBO LA INDIANA (MAREKANI)


Katika Konferensi ya Indiana kule Marekani mnamo mwaka 1900 lilitokea tukio jingine Ambalo lilikuwa la kutisha katika kanisa letu. Baadhi ya Makanisa yetu kule Indiana yalikuwa yakiendesha ibada zikiwa na nyimbo zenye moto wa kigeni. 
Nyimbo hizo zilisikika katika sauti kubwa , zikiwamo ngoma , sauti nzito za vyuma na ghasia zingine. Muziki tena ulio na mchanganyiko wa kishetani ulidhihirishwa katitka makanisa hayo na Roho mtakatifu kwa kawaida asinge tamalaki katika ibada kama ile alisema mjumbe wa Mungu, Ellen G. White. Kufuatia tukio hili la Indiana , Ellen G. White alitabiri ya kuwa hali hii ya Muziki uliojaa makelele na ukiwa na dalili zote za kishetani katika ibada,utaletwa tena katika kanisa la Waadiventista wa Sabato muda mfupi tu kabla ya kufungwa kwa mlango wa rehema.”Sikiliza vile mjumbe wa Mungu asemavyo kufuatia tukio lile kule Indiana: Ibid ., uk 36
“mambo uliyoelezea kutokea kule Indiana, Mungu amenionyesha kuwa Yatarudiwa tena kitambo kidogo kabla ya kufungwa kwa mlango wa rehema.  Kila aina ya vitu visivyofaa vitaachiliwa. Kutakuwepo na makelele, upigaji wa Ngoma kuimba na kucheza. Via vya kufanyia maamuzi vitapumbazwa kiasi Kwamba haviwezi kuaminiwa kufanya uamuzi ulio sahihi na hii itaitwa ni Huduma ya Roho Mtakatifu wa Mungu. Roho Mtakatifu kamwe hawezi Kujidhihirisha kwa njia hii, wala katika sauti za makele kama zile. Hizi ni    Mbinu za shetani za kutweza ukweli. Ni bora kutokuwa na muziki wa jinsi Hii wa kumsifu Mungu kuliko kutumia muziki na jinsi hii ambao mweziJanuary nilijulishwa kuwa muziki huu utaletwa katika mkutano wa Makambi. Ibid. 36

JE KUCHEZA DANSI, VITENDO NA KUMACHI NA MIHEMKO VINA MWONEKANO GANI KATIKA HUDUMA YA UIMBAJI?


Swali la msingi ni hili je kucheza wakati wa uimbaji ni sahihi? (Shall we dance?) Jiibu la swali hili laweza kutokana na kile ambacho kimekwisha onekana katika historia ya Anguko na ukengeukaji wa Muziki kuanzia Edeni, Chini ya mlima Sinai, Baal – Peori mahali Waisrael walipojenga hema hali wakijiandaa kuingia Kanani. Pia walipokuwa wakivuka Bahari ya shamu, Katika Mikutano ya Makambi kule Indiana, Baada ya mwaka 1844, na miaka ya 1990 na kuendelea ambapo imekwisha bainika kuwa Walisrael walipokengeuka  katika kujichanganya na mataifa, kushiriki katika sherehe zao, za ulafi, makelele , kuruka na kucheza kuwa adhabu yake ilikuwa kumbwa na hivyo Mungu hakupendezwa na mtindo wa jinsi hiyo wa ibada. Hivyo basi kucheza dansi hakukubaliki katika ibada takatifu.
Ni muhimu pia kupata ushauri mwingne toka kwenye Biblia juu ya suala hili. Mara nyingi kitendo cha Mfalme Daudi kinatafsiriwa visivyo.  Maandiko ni kweli yanashuhudia kwa maneno yafuatayo: “ Naye Mfalme Daudi akacheza mbele za Bwana kwa nguvu zake zote.”  Mfalme Daudi alicheza sio katika mazingira ya Ibada. Uchezaji wake ulifanyika nje ya ibada ndani ya hekalu, na hiyo inaleta tofauti kubwa.  Kucheza kwa Daudi kulifanyika katika mazingira ya Sherehe ya kushangilia na kushereheka moyoni kwa kuona ya kuwa hatimaye Sanduku la Agano la Bwana limerejeshwa Yerusalemu. ( 2 Sam 6:14, 16 ).
Hivyo basi hapa kuna tukio tofauti na lile ya wakati ibada inapokuwa inaendeshwa katika hekalu.  Miriam na wanawake walishika Makuyamba na wakiimba na kushangilia ukuu wa Mungu wakati alipowavusha katika bahari ya Shamu na kuwashinda Wamisri na jeshi lake walipogharakishwa ndani ya bahari ya Shamu. ((Kutoka 15:1-21)
Wanawake waliimba na kucheza wakati Daudi alipomshinda Goliath (I Sam 18:6,7 ) Binti wa Jephthah aliimba na kucheza alipokuwa anampokea baba yake wakati akitoka vitani kuwaamua waisrael toka kwa maadui zao. (Waamuzi 11:34). Hivyo twaona ya kuwa kucheza dansi kusiwe na uhusiano wakati huduma ya nyimbo inapokuwa inafanyika katika ibada takatifu.
Kufanya Vitendo, Kumachi na Mihemko vinapunguza uzito wa ujumbe ambao umetolewa katika huduma ya uimbaji kwani wasikilizaji badala ya kutafakari ujumbe unaotolewa badala yake usikivu wao unagawanyika kuangalia usanii wa mihemko ya waimbaji, au Maching au usanii wa vitendo  hivi kwa kiasi kikubwa vinahafifisha ujumbe wa mahubiri yanayotolewa na mhubiri wa Kwanza Yaani Kwaya. Hivyo ili kuongeza usikivu wa wasikilizaji ni muhimu ya kuwa wahudumu.Waruhusu ujumbe wao uende kama ulivyotolewa bila ya kuongeza vikorombezo vya vitendo vinavyofikiriwa kuwa vya muhimu. Utukufu kwa Mungu kusudi la Uimbaji
Kusudi kubwa la huduma ya uimbaji nikwa ajili ya kumtukuza Mungu. Mwimbaji anabadilishwa na wasikilizaji pia wanabadilishwa na ujumbe wanaousikia kupitia wa kwaya.  Mawazo yao, huzuni zao, Masumbuko yao, misiba yao, mikasa ya maisha vyote vinakutana na ujumbe wenye matumaini kwa Mungu ambaye kwa kumtumainia aweza kuwachukulia mizigo yao na kuwaweka huru.  Hii ndiyo sababu ni muhimu ujumbe uende kama ulivyo ili mwishoni wasikilizaji wasije wakawatukuza wahudumu kwa ajili ya matendo yanayoonekana kwa macho ya kibinaadamu badala ya kurudisha utukufu kwa Mungu.
Muziki wa kiadiventista unapaswa kuwa na tofauti na muziki unaotolewa na wahudumu wengine ambao sio waadivenstista.  Kwa vile Waadiventista ni watu wa pekee kwa kila kitu. Muziki pia unapaswa uinue bendera ya uadiventista na Kristo atukuzwe katika huduma zao.

MATUMIZI YA VYOMBO VYA MUZIKI KATIKA IBAD

Vyombo vya Muziki vyaweza kutumika katika Uimbaji iwapo mambo ya fuatayo yatatiliwa maanani:
  1.  Mpigaji wa vyombo kwa mfano Piano au Kinanda ni budi awe mtaalamu wa kutumia vyombo hivyo.
  2. Mchezaji awe na Ujuzi wa kusoma Notes na kucheza (Awe mjuzi wa Tonic so lfa na Staff Notation.
  3. Mchezaji asitumie miziki iliyoandaliwa na kuhifadhiwa katika Keyboard au Piano (Ready made Musical accompaniments) Atawale Keyboard au piano au Organ badala ya kutawaliwa na vyombo hivi.
  4. Aepuke Sana matumizi ya sauti ya juu, midundo, ambayo inatisha na kuwafanya watoto wadogo waogope.
  5. Ahakikishe kuwa sauti ya vyombo hivyo, inaruhusu maneno yasikike (lyrics) ambayo ndiyo hasa muhimu katika muziki.
  6. Awe mnyenyekevu, awe tayari kupokea mashauri asiwe na kiburi ambacho ndicho kilileta anguko la Mkurugenzi wa awali ya kwaya ya Mbinguni ambaye hatimaye alianguka kwa sababu ya kiburi chake.
  7. Afahamu jinsi ya kutawala sauti ya vyombo iende sambamba ikiacha nafasi ya maneno kusikika vema (melody, harmony rhythm na balance. ) viende sawia.
  8. Awe tayari kushirikiana na Uongozi wa Kanisa.
Angalizo: Iwapo vigezo hivyo havizingatiwi, ni bora kuimba bila kutumia vyombo vya Muziki.

MAAMUZI YA MKUTANO ULIOFANYIKA KWAKOA (NETCO) MWAKA 2003 CHINI YA IDARA YA VIJANA NA NYIMBO


Mnamo mwaka 2003 kule Kwakoa katika wilaya ya Mwanga, kamati iliyoteuliwa na kupewa majukumu ya kushughulikia maswala ya Nyimbo hasa kuhusiana na matumizi ya Vyombo vya Muziki (Accampaniments) Maamuzi yalikuwa kama ifuatavyo:
      “Watumiaji wa vyombo vya muziki hasa Vinanda ambao hawana ujuzi wa kitaalamu wa matumizi ya vyombo hivyo, Waache kutumia katika kwaya vyombo hivyo hadi watakapokuwa na wataalamu ambao wamejifunza Kusoma na Kucheza vyombo hivyo.Hivyo iliwekwa bayana kuwa kutumia vyombo vya Muziki, Kinanda, au piano ndicho kiwango kinachotakiwa.  Matumizi ya beats au midundo na mapigo vulivyopandikizwa katika Vinanda viachwe kabisa. “
      Konferensi hii chini ya uongozi wa Mchungaji Izungo wakati akiwa Mwenyekiti wa Konferensi wakati huo. Alitoa msimamo ambao ni bora ufuatwe na kitivo cha Muziki cha Kanisa.Unangalifu unahitajika kufanyika katika maeneo haya kwani hii ni sehemu dhabiti ya Msukumo wa Kanisa la Waadiventista wa Sabato ulimwenguni ulio na kauli mbiu ya “Uamsho na Matengenezo.”   John Kimbute, Mwenye kiti wa Kamati ya Muziki wa Konferensi, Kwakoa NETC, 2003.
Kwa Kuzingatia Maamuzi hayo ambayo kwa kiasi kikubwa yamebadilisha na kupunguza kasi iliyokuwepo ya matumizi ya vyombo hivyo kiholela inapokuwa sio kwa makanisa yote bali yapo matengenezo ambayo ni dhahiri. Kwa kuunga mkono maamuzi hayo Samuele Bacciocchi katika kitabu chake kiitwacho: The Christian and Rock Music, anayo haya ya kusema:
      “Viongozi wa Ibada wanaosisitiza utumiaji wa vyombo kadhaa, kama vile Ngoma, Magita    yenye Sauti nzito ya Bass (Bass Guitar) na magita yenye pandikizo la kutoa muziki wa “Rock” katika makanisa yao wanapaswa waelewe ya kuwa kule Yerusalemu katika hekalu  na katika hekalu la mbinguni hakuna vyombo vya jinsi hiyo vinaruhusiwa.” Samuele Bacchiocchi et al   Tha Christian & Rock Music A Study on Biblical Principles of Music. Michigan: Bilbical Perspective,2000) P 177
      “Viongozi wa Ibada wanaoruhusu waimbaji kutumia Ngoma,Magita ya Bass na Magita     ya kuvuma sana ili kuleta sauti ya muziki wa Jazz au rock ni muhimu kwao watambue       ya kuwa katika hekalu la Bwana kule Yerusalemu na pia katika hekalu la Mbinguni.       Hapakuwa na vyombo vyenye sauti kubwa zinazotengeneza (Okestra) katika ibada. Kinyume chake vilikataliwa vyombo aina mbili na vyote vya nyuzi tu ndivyo      vilivyoruhusiwa kutumika katika ibada” Ibid Ni vema pia ieleweke kuwa hakuna kosa lolote kutumia filimbi na Matoazi. Ila vyombo Hivi havikutumiwa kwani vilikuwa vimezoeleka katika matumizi ya miziki ya duniani(Secular Music )  .
       Iwapo vyombo vya muziki vyenye sauti kali vingeruhusiwa kutumika katika ibada, ibada ingebalishwa kuwa mahali pa maburudisho. Hata wanawake Ambao walizoelea sana kucheza dansi hawakuruhusiwa kuwa sehemu ya kwaya. Daudi alichagua wanaume kuwa tu ndio waimbaji.  Hii haina maana kuwa wanawake leo wasijumuishwe katika kwaya isipokuwa iwapo wapo ambao ni wachezaji dansi katika miziki ya kidunia (dance) iwapo hao watafahamika, si vema wahusishwe katika muziki wa kumsifu Mfalme wa utukufu.  Hii ina maana kuwa wale wanaocheza miziki ya kidunia kama kazi wasingeruhusiwa kusimama mbele za mkutano wa watakatifu na kumtukuza Baba wa Utukufu. Hili ni angalizo la muhimu.

NYIMBO ZA KIHOLELA ZIMEHARIBU SURA YA MUZIKI

WA KIADIVENTISTA


  Ili kurejesha sura ya Muziki wa kiadiventista ni muhimu kwaya pamoja na vikundi vya kwaya vizingatie machache yafuatayo:-
  1. Uimbaji upangwe katika Notes  1.  Tonic  Sol fas na 2. Staff Notation
  2. Nyimbo zisiimbwe bila mpangilio kujifunza kwa muda wa kutosha ili zinapoimbwa ziwe zinasikika vizuri.(kwaya ya mfalme Daudi ilifunzwa kwa mda wa miaka mitano)
  3. Ni vema Theme za Nyimbo zetu zizingatie Ujio wa Yesu, Huduma ya Kristo katika patakatifu na Sabato ambalo ni tarajio la pumziko la milele pale Mungu atakapofanya maskani yake pamoja na Wanaadamu.
  1. Kwaya au Vikundi vya Uimbaji viwe na sare inayoelewekaKwani waimbaji  ni wahubiri.-sare ziwe mavazi ya heshima na kusitiri mwili
  2. T shirts zisitumike kama vazi la kusimama mbele ya kusanyiko la watakatifu, na kila aina ya mavazi yanayoweza kuhafifisha huduma ya ibada( isipokuwa katika matukio maalumu)
  3. Waimbishaji wawe na taaluma katika kuongoza nyimbo wafanye bidii katika kujifunza namna ya kufuata mapigo.
  4. Kwaya na Vikundi vyote viandikishwe na kupitishwa na kanisa mahaliaHebu tujifunze kwa kuangalia mfano wa kwaya za mbinguni

MFANO WA MUZIKI WA KWAYA ZA MBINGUNI


Hebu na tujifunze katika kwaya tatu zilizoko mbinguni.  Samuelle Bacchiocchi katika utafiti wake wa Theolojia ya Muziki wa Waadiventista wa Sabato anatujuza kuwa kufuatana na Utafiti wa Oscar Cullman katika kitabu cha Ufunuo kuna kwaya tatu kule mbinguni:- Kwaya ya Wazee Ishirini na Nne (24 ) Ufunuo 4:10 – 11) Mada yao kuu ni kumsifu Mungu kama Muumbaji Wakisema . Wewe Bwana ndiwe  unastahili utukufu, heshima na Uweza, na mwisho wanamsifu Mungu kwa ajili ya wale  waliokombolewa na sifa kwa mwana kondoo wa Mungu ( Wanaimba kutumia Vinubi)  harps).  Yohana anasema,” Nikasikia sauti kutoka mbinguni kama sauti ya maji mengi,  kama sauti ya Ngurumo ndipo nikasikia sauti toka kwa Wapiga vinubi wakipiga vinubi  vyao”( Ufunuo 14;2) Pia wanaimba wimbo mpya (Ufunuo 5:8-9) 
Malaika na Waliokombolewa ambao hesabu yao ni kubwa.  (Ufunuo 5:11-12; 7:9-12)  Mada kuu ni sawa na ile ya Wazee ishirini na Nne Kwaya ya Wote  (Mass Choir) ikihusisha viumbe wote na Waliokombolewa (Ufunuo 5:13) Wakiwa na matawi ya mitende na mavazi meupe.Mada yao kuu ni: Wokovu ni wa Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi na Mwana Kondoo.(Ufunuo 7: 9 – 10)  Wote wanaelekeza sifa na Utukufu kwa Utatu Mtakatifu.
 Kufuatana na Thomas Seel anasema kuwa Kinubi ambacho ni chombo cha nyuzi pekee kinachotumika katika kwaya za mbinguni katika ibada kimepewa kibali kwani ni rahisi kuendana (blending) na sauti za waimbaji.”  IbidYohana wa Ufunuo anatumia neno “Prokuneo” akiwa na maana ya kuwa muziki wa mwisho wa wakati ni muhimu uonyeshe heshima na kicho ili sifa zielekezwe kwa yeye ambaye anastahili,baba wa mbinguni.

HITIMISHO


Mambo makuu (5) ni ya Muhimu kuzingatiwa katika huduma ya Muziki
  1. Muziki wa Kiadiventista ni muhimu uonyeshe heshima na kicho mbele za mahali pa ibada kwani ndio wakati tunakutana na Mungu
  2. Vyombo vya kuzindikiza Muziki vichezwe na wataalamu wa kuvitumia vyombo hivyo na visisikike zaidi na kuzuia maneno ambayo ndiyo yamebeba ujumbe wa Mungu.
  3. Muziki unapotolewa uonyeshe Furaha na uchangamfu wa kuwa mbele za Mungu (Uf. 7:12)
  4. Uwiano uwepo katika Ujumbe unaotolewa na mpangano wa Sauti na ulete somo mahususi linaloweza kueleweka
  5. Waimbaji  wa Kwaya ya Kanisa na Vikundi wawe na sare kadri iwezekanavyo na mavazi ya heshima ya kujiwasilisha vizuri mbele ya watu na Mbele za Mfalme wa Wafalme na Bwana wa Mabwana.
  6. Muziki na huduma ya Uimbaji katika maandiko ni sawa kama Sadaka ya Shukrani kwa Mungu, Ya Uumbaji, ulinzi wa Mungu na Wokovu wa Milele.
  7. Hebu tufanye matengenezo ya kuturejesha katika mapito ya zamani wa Muziki wa Kiadiventista. (Yeremia 6:16.)  Mungu na awabariki.






Saturday 10 May 2014

MALEZI BORA YA WATOTO Na Changamoto ya kizazi hiki





Imeandaliwa na
Mchungaji
 Lupakisyo Mwakobela Mwakasweswe



Barua Pepe:   lmwakasweswe@yahoo.co.uk
Simu ya mkononi: +255- 0764 150 391
Blogi:  Mwakasweswe.blogspot.com

Utangulizi


Katika fundisho hili tutajifunza malezi bora ya watoto katika nyumba za watu wanamwamini Mungu. Ni wakati ambapo wazazi wengi wamekata tama ya mazi ya watoto wao. Kumekuwa na changamoto nyingi kwa jinsi yakuwa lea watoto wanaoishi katika kizazi chetu. Imekuwa kwamba watoto nao wamejifunza na kuiga tabia ambazo wazazi wanashangaa kwamba wametoa wapi? Limekuwa gumzo kanisani kwenye anyumba ya ibada , barabarani , katika taasisi mbalimbali mjadala ukiwa ni jinsi gani watoto wasikuhizi walivyo na tabia za ajabu .
 Kwa kuzingatia umuhimu wa ujenzi wa tabia  mwandishi na mjumbe wa Mungu anaandika katika kitabu cha Elimu ya kikiristo uk 165 anasema “ Ujenzi wa tabia ni kazi ya muhimu kuliko zote alizopewa mwanadamu; na kamwe kabla umuhimu wa kujifunza kanuni kwa makini haujakuwapo kama ulivyo sasa.”
 Katika somo hili tutajifunza mpango wa Mungu kwa uzazi wa watoto, pia  tutajifunza na kuona wapi tumefanya makosa kama wazazi katika ujenzi wa tabia za  watoto wetu.
Malezi ya watoto hayakosi changamoto ambazo wazazi wanakutana nazo, yaweza kuwa kupitia maisha na tabia walizojifunza kutoka kwa marafiki yaani makundi au kwa kuzipata kupitia malezi ya wazazi wao. Changamot hizi ni pamoja na watoto kujiingiza katika unywaji wa pombe, kuacha maisha ya ibada, kuvuta sigara na bangi, kuwa na mahusiano ya kingono kati ya jinsia mbili na jinsia moja yaani ushoga, kutopenda masomo, kuwa na ujauzito usio halali, magonjwa ya zinaa na Ukimwi.
Somo hili halitajadili maendeleo ya mtoto katika ukuaji wake bali  litazungumzia malezi bora ya ujumla kwa watoto. Ni tumaini langu kwamba baada ya somo hili, kila Mzazi atajua wajibu wake kwa malezi bora ya watoto wake, kila mzazi atahisi mahali alipo fanya vibaya katika malezi ya watoto wake pia atafanya yampasayo kutenda  ili kuwa na  malezi bora ya watoto wake.

Mpango wa Mungu kwa wazazi;  Adamu na Hawa


Mwanzo 1:27,28  Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. 28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi. Mpango wa Mungu  ulikuwa kumuumba mwanadamu kwa mfano wake, na kwa maana hiyo mwanamke na mwanaume  ni mfanao wa Mungu.

Unaweza kujiuliza kwamba Mungu anafanana na mwanamke au mwanaume, hilo si swala la kujadili kwani Mngu anaumba mtu kwa namna yake ya asili. Mwanadamu ameumbwa akiwa mkamilifu katika njia zake mpaka pale dhambi ilipo ingia na kumfanya mwanadamu apoteze sura ya ukamilifu wa Mungu.

            Mungu alifahamu kwamba hawa wazazi wangekuwa mfano bora katika maisha yao mbele ya watoto wao, watoto wasingehangaika kuyafamu yaliyo mapenzi ya Mungu. Tunayo furaha kwamba baada ya anguko la mwanadamu Mungu alifanya mpango wa ukombozi, Yesu kristo akaja akafa badala ya mwanadamu, mwanadamu akahesabiwa kwamba ana haki kwanjia ya Yesu kristo. Yohana 3:16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.Wazazi wanaqodumu kuwa waaminifu wameahidiwa kuto potea bali wamehakikishiwa uzima wa milele.

Katika kitabu cha mwanzo 1:27, 28 Mungu akawabarikia wazazi wetu wa kwanza, Mungu akawapa wajibu wazazi wetu wa kwanza , wazazi hawa alipewa kila kitu kilcho kuwa muhimu kwa maisha yao. Mungu anajuwa kilicho muhimu katika maisha yetu pia, aliweza kuwapatia wazazi hawa vitu maalumu vya kula hata vya kutunza tu, kisha baada ya kuwabarikia, biblia inasema Mungu akawaambia, Zaeni .
Kuzaa ni agizo la Mungu tangu katika bustani ya edeni, kuzaa ni agizo baada ya kubarikiwa, unaweza kugundua kwamba Mungu hakutoa agizo la kuzaa mpaka kwanza alipo wabariki wazazi wetu, Mungu aliwapa vitu muhimu vizuri vya kuwa navyo kabla ya kuzaa. Mungu wetu ni Mungu wa utaratibu, hachanganyi mambo kama ambavyo mwanadamu anachanganya mambo, hebu angalia, mzazi anajikuta ni mjamzito bila kujua nini cha kumpatia motto anayetarajiwa kuzaliwa.
Siyo ajabu wazazi wengi wameanza maisha bila kuju kwamba Mungu amewabariki kwa kuwa na vitu vya kuanzia maisha hasa watoto wanapo anza kuja duniani, hebu fikiri mzazi, Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, zaeni. Je kabla ya kuzaa ulijiandaa kiasi gani kuhusu maisha ya motto au watoto wako? Mungu hatoi agizo la kuzaa kabla ya kukubariki.
Wazazi wengi wameiga kutoka kwa wazazi wengine na kusema kila motto huja na bahati yake, hili limesababisha watoto wengi wamezaliwa katika mazingira ya hatari sana, wengi hawajakutana na nepi kama wengine wengine wamektana na vipande vya kanga nk. Agizo la Mungu ni kubariki na kutoa agizo la kuzaa. Agizo la kubariki tumbo la uzazi liko palepale lakini hakuagiza uzazi usio na mpango. Mungu anapoagiza, Mkaongezeke , alimaanisha vizazi na vizazi na kuongezeka kwa namba ya wanafamilia yako nay a jirani yako, pia alimaanisha Kujaza nchi, Mungu anapendezwa na watu wanoweza kumwabudu kumsifu. Mungu alijua watu wengi watakuwepo ambao watatangaza habari zake katika ulimwengu huu. Mimi na wewe mzazi ni matokeo ya ongezeko la watu duniani.
Kwa taarifa ya sensa ya mwaka  2012 Watanzania tumefikia idadi ya watu 42,000,000( milioni arubaini na mbili) ongezeko hilo ni changamoto kwa serikali na kwa familia, kwani linatakiwa ongeko la miundo mbinu, chakula, maji, barabara , makazi mazuri , mpango mzuri wa uzazi, Magonjwa ya wakina mama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano nk.
Agizo la  Mungu kwa wazazi wetu wa kwanza  ,waliambiwa waweze kuitiisha nchi  Mwanzo 1:28  na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi. Wajibu huu mkubwa wa kutiisha ni wajibu wa kila mzazi, kuhakikisha kwamba vinatii maagizo yako, kutawala na kuhakikisha kila kiumbe kiendacho juu ya nchi kinatawaliwa nawe, si ajabu ukashangaa kwamba viumbe wengine ambao bado hawajazaliwa utakuwa na wajibu wa kuhakisha maisha yao yanatunzwa vizuri na wewe, zaidi sana wewe kama mzazi ndiye unaweza kutiisha hata ujauzito ukatungwa kipindi utakacho panga, kumbe kama mzazi utakuwa tayari kuendelea kumpatia elimu ya Mungu mtoto wako uliye mzaa.
Bahati mbaya wazazi wengi tumewaleta watoto duniani bila utaratibu na kujenga hoja kwamba bado nina nguvu za uzazi na mayai bado yapo, hilo ni sahihi kabisa lakini tukasahau kwamba Mungu wetu ni wa utaratibu, anabariki kwanza na anatoa agizo kwamba Zaeni. Unaweza kupita mitaani na usishangazwe na majina ya watoto kama vile Sikujua, Mapenzi , Yote haya ni kujipa matumaini kwamba Mungu alipanga mtoto huyu azaliwe pasipo kujua, na wakati mwingine tumeseam ni mapenzi ya Mungu, yote hayo ni sawa lakini tiukumbuke kwamba Mungu ni Mungu wa utaratibu.
Ninajaribiwa kuamini kwamba ilipo fika wakati wa kugawa mali kwa wtoto, wazazi wetu wa kwanza hawakupata tabu kwa sababu kila kilicho kuwa hitaji la mtoto lilifanyika. Mwanzo 4:2 Akaongeza akamzaa ndugu yake, Habili. Habili alikuwa mchunga kondoo, na Kaini alikuwa mkulima ardhi. Hebu chunguza hapa kwa makini, Baada ya wazazi wetu kuongeza motto , Habili alikuwa mtaalamu wa mifugo na Kaini alikuwa mtaalamu wa Shamba. Wazazi hawa walipoombwa mali Ninaamini walitoa kwa moyo wote, Habili walimpatia kondoo za kumtosha , na kaini walimpatia eneo kumbwa la ardhi.

Watoto ulionao na unaopanga kuwaleta duniani  wanacho kitu cha  kuwatosha kutoka kwako? Umebarikiwa kiasi gani kuweza kuwaridhisha watoto wako. Unauelewa kiasi gani wa neno la Mungu kama mafundisho awali kwa watoto wako, umejiandaa kiasi gani kwa malipo ya ada ya shule na vyuo, unamaandalizi kiasi gani ya Vyakula katika nyumba yako.

 Mungu wetu anautaratibu mzuri. Tambua mbaraka wako kabla ya kuzaa. Mwandishi E.white akieleza habari hii anasema   “Wako wazazi  ambao, bila kufikiri kama waweza kuwatendea ipasavyo jamaa kubwa ama sivyo, huzijaza nyumba zao watoto hawa wadogo wasioweza kujisaidia wenyewe, wenye kuwategemea tu wazazi wao kwa matunzo na kwa mafundisho. Hili ni kosa kubwa baya, si kwa mama tu, bali kwa watoto wake na kwa jamii ya watu mtaani. Mtoto mikononi mwa mama mwaka kwa mwaka ni udhalimu mkuu kwake. Hupunguza , na mara nyingi huharibu starehe na kuongeza uchovu wa kazi nyumbani. Huwanyang’anya watoto matunzo, elimu na furaha amoto ulimwenguni ambayo wazazi wangeiona kuwa ni wajibu wao kuwapa  (Wazazi) wangefikiri kwa makini riziki wawezazo kuwapatia watoto wao. Hawana haki kuzaa watoto ulimwenguni kuwa mzigo kwa wengine”.  AH 159 - 164

Wazazi wengi wamejikuta wakiwatukana watoto wanapohitaji mambo muhimu ya shule. Nilishuhudia mzazi mmoja akiombwa na motto wake penseli ya kuandikia shuleni naye akamjibu kwamba “wewe unadhani si tunakunya hiyo penseli”. Niliamua kunyamaza ila niliumia sana, je motto amliumia kiasi gani? Unadhani mapenzi ya mtoto huyo kwa mzazi wake huyo yakoje sasa.

Wazazi wengi wamepandikiza tabia mbaya kwa wtoto wao kwa jinsi walivyo walea katika maisha yao ya utoto. Watoto wengi walijibiwa vibaya na kupigwa kwa sababu ya wazazi kukosa vitu au mali kwaajili ya kusaidia elimu ya watoto wao. Mungu anampango mzuri kwako wewe unayaendelea kuzaaa au unaye anza kuzaa, Panga uzazi wako maana Mungu anabariki kwanza ndipo anaagiza mwanadamu azae

 Malezi bora yanaendana na mpango mzima wa maandalizi ya ujauzito na kuendelea kulea katika njia njema. Tabia njema zitafundishwa kwa watoto endapo mzazi utafahamu maendeleo ya tabia za watoto kutokana na mazingira ya kurithi na katika mazingira.

Malezi na Tabia za watoto kwa kurithi


Kumekuwa na changamoto kubwa sana kwa wazazi katika kurekebisha tabia za watoto wao ambazo ni matokeo ya kurithi. Watoto wengi wamezaliwa na tabia za wazazi wao au babu zao , kwa mfano hali za moyo, akili, tabia za maumbile ya nje  kwa mfano rangi za macho na ngozi, mfumo wa meno, urefu, uzito, pamoja na mihemuko.
 Mara zingine motto anaweza kuwa hajiwezi darasani ,hii inaweza kuwa sehemu ya kurithi, hii yaweza kusababishwa na mambo mengi ambayo yanahusiana tangu utungaji wa mimba na malezi baada ya hapo. Maandishi ya liyovuviwa  yanasema “ Ikiwa kabla ya kuzaliwa mtoto wake, mama mwenyewe ni mfisadi, kama ni mchoyo, mwenye harara na mkali, tabia hizi zitaonekana kwa mototo . Hivyo watoto wengi wamerithi maelekeo mabaya wasiyoweza kuyashinda ila kwa shida sana “AH 255 -267                                                                                                
Kwa namna nyingine , mzazi asingeharakisha kutoa adhabu kwa motto wake kabla ya kukaa na motto wake na kumweleza makosa yake. Mara zote isinge kuwa bora kuadhibu bila kujua kwamba ulifundisha jambo unalolichukia kwa motto wako, endapo amejifunza kutoka nje yako, pia ni vyema ukajiridhisha na kujua jinsi ya kuongea naye. Maandishi ya uvuvio yanasema “ Akili za watoto ni nyepesi, nao hutofautisha sauti za uvumilivu, na upendo na amri kali ya hasira, ambayo hukausha upendo na nia njema mioyoni mwa watoto. Mama Mkristo wa kweli hatawafukuza watoto wake machoni pake kwa ukali wake na kukosa huruma. “AH 232 -254

Malezi Na Tabia za watoto kutokana Na Mazingira

Sababu za Maombi katika Familia

            Kama kuna jambo la muhimu katika familiani suala la ujenzi wa tabia watoto kwa kupitia Nen la Mungu. Mithali 22:6 Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mze.   Kumbukumbu la Torati 6:7 nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.Kumbukumbu la Torati 11:19 Nayo wafunzeni vijana vyenu kwa kuyazungumza uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.
Wazazwote wangefuata mashauri haya , watoto wengi wangaliweza kuwa na maisha bora, lakini hujachelewa ” Baba na mama, kila siku asubuhi na jioni wakusanyeni watoto wenu karibu  nanyi, kwa maombi ya unyenyekevu, inueni mioyo yenu kwa Mungu mpate msaada.” 7T 32-44

Sababu za kiuchumi

            Wazazi wengi wamekuwa wakijishughulisha na maswala ya kiuchumi ili kukidhi mahitaji ya watoto wao. Imekuwa kwamba wazazi wengi wameshughulika lakini matokeo yake yamekuwa hafifu hata kushindwa kutosheleza mahitaji ya watoto wao. Hii yawezekana kwa kukusa kujituma (uvivu) kutokuwa na maarifa ya kubuni njia za kupata fedha za kutunza familia zao.


Taifa la Tanzanai akwa ujumla limekuwa likisisitiza kuhusu elimu ya ujasilia mali ambayao inamfanya mtu kuwa mbunifu na kuanza kufanya kitu , kwa uchache sana wengi wamepuuza elimu hii na wamebaki wakiwa na sababu za kutokuwa na mali za kulea watoto wao, hii ni makosa kwa mzazi.
            Sababu za kiuchumi zinahusisha ni kwa jinsi gani mzazi umefanikiwa kuwa na kipato chako binafsi, kuwa na uwekezaji, utunzaji wa fedha kwa ajili ya matumizi ya baadaye,kuwa na madeni ambayo yamesumbua familia nyingi hata kukosa mahitaji muhimu, kukosa katika hili kumewafanya wazazi wengi kukusa vitu muhimu yaani chakula bora, afya nzuri ambavyo ni muhimu sana kwa ukuaji wa mototo.
            Maandishi ya uvuvio yanaeleza kwamba “Watu wengi walio maskini ni maskini kwa sababu hutumia fedha zao mara tu wazipatapo” AH 392
 Akiendelea anasema “Wale wanajidai Kwa hali yoyote kuwa wenye utauwa, yawapasa kujivika mafundisho wanayo yakiri, wala wasitoe nafasi kwa neon la Mungu hutukanwa kwa sababu ya mwenendo wao wa kutojali. Mtume anasema, “ Msiwiwe na mtu cho chote” 5T179 – 182

Sababu za mlo

Sababu za kukosa chakula chenye viini lishe, wazazi wengi wamejikuta watoto wao wakiwa na tabia tofauti katika makuzi yao. Kukosa mlo kamili ni kosa kubwa katika malezi ya watoto. Hata Tanzania , tumebarikiwa kuwa na chakula cha mboga  matunda ,nafaka, vyakula ambayo  kama vingetumiwa vizuri vingeweza kusaidia katika makuzi ya watoto na ujenzi wa tabia njema. Magonjwa mengi kama vile kuishiwa damu , utapiamlo , na magonjwa mengine vimechangia sana katika maendeleo mabaya  ya ukuaji wa akili za watoto.
 Tabia za watoto wengi zimeharibiwa na jinsi walivyp lelewa na kwa jinsi walivyo achwa hivyo , leo tunaweza kushuhudia watoto wengi hata watu wazima wakifanya mambo tofauti kwa sababu tu ubongo wao haukuandaliwa vizuri katik aumri wao mdogo.

Sababu za Magonjwa na  kuugua

            Watoto wengi wameathirika akili zao Kwa kuwa na magonjwa ambayo yameathiri akili zao, mihemuko yao na makuzi ya kijamii. Magonjwa Kama ya mifupa, baridi yabisi, kuwa na usumbufu wa kutosikia vizuri. Yote haya yanasababisha tabia za watoto ziwe tofauti na makusudio ya mzazi.
 Inapasa wazazi kuwa makini katika kujikinga na magonjwa mbalimbali yanayoweza kunyemelea watoto wako. Wazazi wengi wamepuuzia kuwapeleka watoto wao katika hosipitali, kumekuwa na matangazo mengi ya kupeleka watoto kwenye chanjo lakini ni wachache wanao itikia mwito huu. Hebu kila mzazi atambue wajibu wake.

Sababu za Mazoezi ya Viungo

            Mazoezi ya viungo ni dawa nzuri Kwa afya yakila mtu. Watoto wanafaidika Sana kwani mazoezi yanasaidia kupunguza msongo wa maisha, yanasidia katika kujiamini, kuosa mazoezi kumefanya watoto wengi kudumaa, wamejikuta afya zao zikiwa mbaya, wameshindwa kukuwa kwa ulinganifu uliobora.

Sababu za Mila na Desturi za jamii.

            Katika eneo hili, tamaduni zimechangia kutengeneza tabia za watoto, kwa mfano jamii nyingi zimekuwa na ubaguzi wa jinsia.
 Kwamba watoto wakiume wamechukua sehemu ya juu sana na kuonekana wanafaida kubwa katika jamii kuliko wana wa kike. Watoto wengi wa kiume wamekuwa wakishindwa kufanya kazi ndogo za nyumbani kwa kutegemea kuwapo kwa wasichana. Watoto w kike wameshindwa kupata elimu kwasababu wazazi wengi wanadhani watoto wa kike ni wa kuolewa tu. Maandiko matakatifu katika kitabu cha Mathayo 25:40 Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi. Swali kubwa Kwa wazazi leo, tunawafundishaje watoto wetu katika mila na desturi zetu? Tabia zao zinaathirika kwa kiasi gani? Yesu anasema kwa kutenda kwetu.
 Hii imefanya tabia za baadhi ya watoto wa kike kutojiamini katika maisha yao na kujiona kwamba wao ni wa kuolewa tu hivyo huanza tabia za kutafuta kuolewa hata kabla ya umri unafaa. Wazazi wangejifunza kwamba Mungu hana Upendeleo wala ubaguzi. Kwa kufanya hivi ni kumkosea Mungu.
Tamaduni hizi zimekumba nyumba za ibada. Wazazi walio wafundisha watoto wao kwamba wao hawafai kusimama mbele za wana wa kiume mpaka sasa wamekuwa na tabia ya woga, wa meshindwa kushiriki kikamilifu katika kazi za kanisa na shughuli mbalimbali za mahali pa ibada ya Mungu. Tabia hizi ni matokeo mabaya ya kuwa na tamaduni ambazo hazina ukubali wa maandiko matakatifu ya Mungu kwani Mungu alipoumba mwanadamu alitaka kila mtu amwabudu yeye.  
Maandiko matakatifu katika kitabu cha Ufunuo wa Yohana 14:7 akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji
Hakuna aliyeachwa katika kusujudu mbele za Mungu, hakuna aliyeachwa katika kumcha Mungu na kumtukuza kwa sababau hukumu italetwa kwa kila mtu, haijalishi ni jinsia ya kike au ya kiume, hivyo basi tamaduni mila na desturi zisifanye wazazi wengi kuwafundisha watoto tabia zitakazo haribu maisha na wokovu wao.

Changamoto za malezi ya watoto katika kizazi hiki

 Unywaji wa pombe ,Katika ulimwengu huu wa sayansi na technolgia, kuacha maisha ya ibada, Uvutaji wa sigara, bangi,( madawa ya kulevya) kuwa na mahusiano ya kingono kati ya jinsia mbili na jinsia moja yaani ushoga, kuwa mtoro wamasomo, kuwa na ujauzito usio halali na kupata Magonjwa ya zinaa na Ukimwi.
Pamoja na changamoto hizi, mzazi anapaswa kumwombea motto wake ili kwamba Mungu aepushe balaa hizi. Wakati Fulani unaweza ukapatwa na majaribu kwamba mtot wako amejiingiza katika moja wapo ya hayo, kumbuka endapo ulimkabidhi mikononi mwa Mungu, Mungu bado anazungumza pamoja naye maana hata acha mafundisho aliyopewa na mzazi hata atakapo kuwa mzee. Endelea kuomba na akuomba na kuomba.